December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mashbiki wenye hasira kali wa klabu ya Barcelona wamekusanyika nje ya ofisi ya klabu hiyo wakishinikiza mchezji wao Lionel Messi abaki

Mashabiki Barcelona wamtaka Messi abaki

BARCELONA, Hispania

MASHABIKI wenye hasira wa klabu ya Barcelona wamekusanyika nje ya ofisi za klabu hiyo wakimtaka mchezaji mahiri wa timu hiyo Lionel Messi aendelee kusalia kwenye timu yao kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Hispania La Liga na michuano y Kimataifa.

Hata hivyo, mashabiki hao wamemtaka Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu kujiuzulu baada ya habari kuvuja kwamba Messi ameiambia klabu hiyo anataka kuondoka.

Messi, mwenye umri wa miaka 33 raia wa Agentina, ameifungia timu hiyo mabao 634 kwenye mechi 737, ​​lakini wakati wake sasa umefikia mwisho, baada ya kuwasilisha maombi ya kutaka kuondoka kama mchezaji huru kulingana na vipengele kwenye Mkataba wake.

Hata hivyo, mashabiki wa klabu hiyo waliokusanyika nje ya ofisi huku wakiimba kwa kumtaka asalie ndani ya timu yao kutokana na mchango mkubwa alioutoa.