December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Masele afunguka baada ya kutoswa Ubunge Shinyanga Mjini

Kikao Cha Halmashauri Kuu  Ya CCM Taifa (NEC) jana  baada ya kuwatangaza  Majina ya Wagombea Ubunge kwenye Majimbo watakaopeperusha bendera ya Chama hicho katika uchaguzi Mkuu 2020.

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Stephen Masele ambaye aliongoza katika uchaguzi wa kura maoni CCM kwa kura 152,  amesema amepokea kwa heshima maamuzi ya chama chake kwa kumtangaza Patrobas Katambi aliyeshika nafasi ya 7 kwa kura 12 katika kura za maoni kuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini katika uchaguzi mkuu 2020.

“Nimepokea kwa heshima kubwa maamuzi ya chama changu, nawashukuru wananchi wa jimbo la Shinyanga Mjini, viongozi wote wa chama changu ngazi zote kwa kunipa fursa ya kuwa mbunge kwa miaka kumi, tushikamane kukipigania chama kiweze kushinda uchaguzi mkuu, binafsi nitashiriki kikamilifu” Stephen Masele.