Na Penina Malundo,Timesmajira Online
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema filamu ya “The Royal Tour” iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanikiwa kwa kiwango kikubwa na kwamba kwa sasa watalii wameongezeka.
Masanja ameyasema hayo Jana Julai 11,2023 alipotembelea Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea Jijini humo.
“Tunatambua kwamba ni nadra sana kumpata Kiongozi anayeamua kuongoza kwa vitendo kama alivyofanya Rais Samia, ametangaza kwa vitendo vivutio vyetu hivyo tunatakiwa kuvitembelea vivutio hivyo ili kumuunga mkono”, Masanja amesisitiza.
Masanja ametumia nafasi hiyo kuwahimiza Watanzania kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko nchini akitolea mfano wa maeneo ya Malikale, Misitu ya Asili, tamaduni za Kitanzania, historia za Tanzania za Waasisi wa Taifa na maeneo mengine ya utalii.
“Tutembelee vivutio vyetu, ukishakitembelea kile kivutio unakuwa umechangia pato la Taifa lakini hata wewe mwenyewe utakuwa umejifunza historia ya nchi ilivyo lakini pia utapunguza hata msongo wa mawazo” Mhe. Masanja amefafanua.
More Stories
Mwanasiasa mkongwe afariki Dunia
Rais Samia Kuzindua Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM