Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Ilala
NAIBU Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar-es- Salaam Ojambi Masaburi ,ambaye ni Diwani wa Kata ya Chanika amesema,ameahidi kuchangia kiasi cha milioni 10 Benki ya Wanawake wa Kata hiyo, katika ufunguzi unaotarajia kufanyika Mei mwaka 2025.
Masaburi,ametoa ahadi hiyo leo katika ufunguzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi la Kata ya Chanika lenye mitaa nane.
“Jukwaa la wanawake Chanika nimesikia SACCOS yenu mnakopeshana wenyewe kwa wenyewe kwa hisa zenu, mmepiga hatua na kuunga juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan,za kuwezesha wanawake kiuchumi mfungue benki, na nitawachangia milioni 10 siku ya ufunguzi wake,”amesema Masaburi.
Amesema faida ya kufungua benki watu walikopa riba inabaki katika akaunti faida inakuwa kubwa na mitaji inaongezeka.
Pia amewasisitiza kushikamana na kuwa wa moja katika jukwaa hilo, ili malengo yao yaweze kutimia ambapo kauli mbiu ya siku ya mwanamke Duniani kata ya Chanika inasema”Kuzaliwa mwanamke sawa na digrii moja ya chuo kikuu”.
Katika siku ya Wanawake Chanika Naibu Meya Ojambi Masaburi alikata keki ya wanawake kwa 500,000 huku akiwaahidi wanawake waliotimiza taratibu za mikopo ya asilimia 10, inatolewa na Halmashauri watapata milioni 100 kupitia vikundi vyao.
Katibu wa Jukwaa hilo Frola Chacha ,amesema Jukwaa la Chanika lilizinduliwa mwaka 2023, likiwa na wanachama 200 na sasa wapo 300,huku dhumuni ni kujenga uwezo katika nyanja mbalimbali zinazohusiana na mwanamke, kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Frola amesema wamefanikiwa kuwaunganisha wanawake na kuwahamasisha kushiriki katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi na wameweza kuwaunganisha wanawake,vijana na watu wenye mahitaji maalum kujiunga katika vikundi ambapo hadi sasa vipo vikundi 50,ambavyo vimesajiliwa kati ya hivyo 35 vimeshaomba mikopo.
More Stories
Nachingwea waanza kuona manufaa vituo vya kudhibiti wanyamapori waharibifu
Ajuza aileza timu ya msaada wa kisheria anavyonyang’anywa urithi kisa kuzaa watoto wa kike
DC Mpogolo awataka wenyeviti wa mitaa kusimamia usafi