Na Severin Blasio, TimesMajira Online
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Martine Shigella amepiga marufuku Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kutumiajeshi la akiba (mgambo) katika ukusanyaji wa mapato badala yake watumike kulinda majengo.
Shigella ametoa agizo hilo ikiwa ni siku chache baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheila Lukuba kwa tuhuma za askari hao kuwapiga wafanyabiashara wa mbogamboga wakidaiwa kufanya biashara kinyume cha sheria.
“Kuanzia muda huu naagiza wakurugenzi wote kuwa sitaki kusikia operesheni ya kutumia mgambo kuwabughudhi wafanyabiashara ndani ya mkoa huu.Kama mnawahitaji askari hao,watumie katika kulinda majengo yenu,na siyo kuwatumia katika ukusanyaji wa kodi,”amesema Shigella.
Aidha, Shigella ametoa agizo la kupunguza tozo mbalimbali katika soko la Kingalu zikiwemo za vizimba,vioski,wauza mitumba huku akifuta tozo za bodaboda na bajaji kwa lengo la kuwavutia wafanyabiashara ambao walikimbia soko hilo na baadhi yao kuanza kupanga bidhaa kando ya barabara.
More Stories
Madiwani Ilala watoa chakula kwa watoto yatima
Waziri Mkuu: Tumieni matokeo ya tafiti za kisayansi katika utekelezaji wa mipango ya kitaifa
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano