Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
MSANII wa muziki wa Bongo Flava, Omary Ally Mwanga, maarufu kama ‘Marioo’, ametambulishwa rasmi kuwa Balozi wa Bahati Nasibu ya Taifa ya Tanzania.
Ushirikiano huo wa kimkakati unaleta matumaini, burudani, na fursa zinazoweza kubadilisha maisha ya Watanzania.Huku Bahati Nasibu ya Taifa ikikaribia kuzinduliwa rasmi, Kampuni ya ITHUBA.
ITHUBA, mwendeshaji rasmi aliyepewa dhamana ya miaka nane, inaleta enzi mpya ya ushindi ambapo kuamini katika uwezekano wa kitu kunageuza ndoto kuwa uhalisia.Katika kiini cha bahati nasibu yenye kauli mbiu “Amini. Cheza. Ushinde.

Akizungumzia jukumu lake jipya kama balozi wa Bahati Nasibu ya Taifa, Marioo hakuweza kuficha furaha yake:”Nina furaha kubwa kutangaza kuwa mimi sasa ni balozi rasmi wa Bahati Nasibu ya Taifa! Huu ni wakati mkubwa, sio tu kwangu kama msanii, bali kwa kila Mtanzania anayethubutu kuota ndoto kubwa.
“Bahati Nasibu ipo hapa kufungua milango, kutengeneza washindi, na kuinua jamii, nami najivunia kuwa sehemu ya safari hii. Ushirikiano huu unamaanisha kwamba ushindi si ndoto tena bali ni uhalisia unaosubiri kutokea,” amesema Marioo.
Naye Mkurugenzi kutoka ITHUBA Tanzania, Kelvin Koka, amesisitiza kuwa ushawishi wa Marioo unamfanya kuwa kiungo bora kati ya burudani na michezo ya kubahatisha.
“Marioo ni zaidi ya msanii, yeye ni alama ya kizazi kipya cha Watanzania wanaothubutu kuamini katika ndoto zao. Nguvu yake, uhalisia wake, na uhusiano wake wa karibu na mashabiki wake vinamfanya kuwa balozi sahihi wa Bahati Nasibu ya Taifa.

“Kupitia yeye, tutahamasisha Watanzania wengi zaidi kushiriki kwenye michezo ya bahati nasibu ambayo ni ya haki, ya kusisimua, na yenye uwezo wa kubadilisha maisha,” amesema Koka.
“Lakini Bahati Nasibu ya Taifa haihusiani tu na ushindi binafsi—ni chombo cha maendeleo kinachowekeza katika miradi ya michezo ili kuinua vipaji na kusaidia jamii.
“Tumejidhatiti katika uwazi, ubunifu, na michezo inayowajibika. Kila tiketi inayouzwa inachangia maendeleo ya taifa, kuhakikisha kuwa washindi si watu binafsi pekee bali ni Watanzania wote kwa ujumla,” ameongeza Koka.
“Ushirikiano wa Marioo unazinduliwa kwa kampeni kubwa za kitaifa, matukio ya kusisimua, na jackpots za kiwango cha juu ambazo zitawageuza mashabiki wake kuwa washindi,”.
ITHUBA Tanzania iko tayari kuandika historia, ikibadilisha kila siku ya kawaida kuwa siku ya ushindi kwa kila Mtanzania, kwa kutumia hashtag rasmi #BahatiNasibuYaTaifa na #Inakuja, Bahati Nasibu ya Taifa inalenga kuongeza ushiriki wa kidijitali na kuwahamasisha Watanzania kote nchini kushiriki.


More Stories
Madiwani waomba Jimbo la Korogwe Vijijini ligawanywe
Dkt.Nchimbi:Watoa rushwa hawatakiwi CCM
Dkt.Diallo:Nunueni pembejeo mapema baada ya kuuza mazao