Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online DSM
Ubalozi wa Marekani umetoa mafunzo kwa askari wa Jeshi la Polisi Nchini yanamna ya kukabiliana na matukio ya kughushi nyaraka mbalimbali ikiwemo hati za kusafiria(Pass Port) ambapo mafunzo hayo yamehusisha wakufunzi kutoka chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA).
Akiwapongeza na kuwapa vyeti vilivyotolewa na ubalozi wa marekani leo April 18.2023 Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi Daktari LAZARO MAMBOSASA amesema vyeti hivyo ni alama ya kile walichosoma kwa lengo la kusaidia Jeshi katika maswala ya kupambana na uhalifu wa kughushi nyaraka mbalimbali.
Aidha Daktari mambosasa amewataka wahitimu hao kutumia mbinu walizopata katika mafunzo hayo yaliyotolewa na ubalozi wa marekani ambapo amesema kuwa taifa hilo liko mbele kiteknolojia nakuwaomba watoe mbinu hizo kikamilifu kwa askari ambao watakuja kupata elimu hiyo.
Kwa upande wake kamishina msaidizi wa Polisi hamisi Msolo ambaye ni miongoni mwa walio hitimu elimu hiyo amesema kuwa wanamshukuru Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP CAMILIUS WAMBURA kwa namna alivyojenga uhusiano na ubalozi huo na kuleta mafunzo muhimu katika kipindi hiki cha mabadiliko ya sayansi na teknolojia ambapo amebainisha kuwa mafunzo hayo yanakwenda kuleta tija kwa watendaji wa Jeshi hilo.
Nae mkaguzi Msaidizi wa Polisi Samweli Maimba ameushukuru uongozi wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam kuwapatia na fasi hiyo muhimu ambapo amebainisha kuwa kutokana na mafunzo hayo yamewajengea uwezo mkubwa wakufunzi wa chuo hicho.
More Stories
Tanga kutumia vituo 5405,kupiga kura leo
NMB yatoa msaada wa vifaa Mufindi
Viongozi wa dini Katavi waomba wananchi kujitokeza kupiga kura