January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Joe Biden kupeperusha bendera ya Democratic urais Marekani.

Joe Biden ameidhinishwa rasmi kuwa mgombea urais atakayepeperusha bendera ya chama cha Democratic mwaka huu huku kukiwa na hotuba za kusisimua kutoka kwa waliowahi kuwa viongozi wa taifa hilo.

Wawili waliowahi marais wa Marekani kupitia chama cha Democratic, Bill Clinton na Jimmy Carter, pamoja na aliyekuwa Waziri wa mambo ya nje Colin Powell, wa chama cha Republican, wamemuidhinisha rasmi Bwana Biden.

Clinton amesema ofisi ya Rais Donald Trump imesababisha vurugu wakati wa uongozi wake wa kipindi cha miaka mitano

Hata hivyo Trump mpaka sasa anamuongoza Bwana Biden katika kura ya maoni kabla ya uchaguzi wa Novemba mwaka huu.

Hii ni mara ya tatu kwa Biden kuingia kwenye kinyang’anyiro cha urais huku mwakilishi huyo wa chama cha Democratic akionekana kuwa katika kipindi cha mabadiliko makubwa ikizingatiwa kwamba kampeni yake ilionekana kuwa katika hatari ya kupotea mnamo mwezi Februari.

Usiku wa pili wa mkutano wa chama hicho Jumanne, mada ikiwa ni masuala ya uongozi, Clinton alitoa hotuba ya kilele.

“Donald Trump anasema tunaongoza duniani,” Clinton amesema katika hotuba yake ya dakika tano iliyorekodiwa akiwa nyumbani kwake Chappaqua, New York. “Sisi ndio nchi pekee iliyostawi kiuchumi ambayo kiwango cha waliokosa ajira imeongezeka mara tatu.

“Wakati kama huu, Ikulu inatakiwa kuwa kitovu cha kila kitu. Badala yake ni kituo cha dhoruba. Kinachopatikana huko ni fujo na ghasia pekee.”

Kufuatia hotuba ya aliyekuwa mama wa kwanza wa taifa hilo Michelle Obama na Seneta Bernie Sanders Jumatatu, hotuba za Jumanne zililenga kuonesha wapiga kura vile chama cha Democratic ndio kilicho katika nafasi nzuri zaidi ya kurekebisha matatizo yaliyopo nyumbani na nje ya nchi.

Powell alisema Bwana Biden ana maadili “niliyojifunza wakati ninakua huko South Bronn na nikiwa mwanajeshi”.

Alisema kwamba anamuunga mkono kama rais kwasababu “tunahitajika kurejesha maadili hayo katika Ikulu ya Marekani”.

Mwezi Juni, Powell – ambaye alihudumu chini ya uongozi wa Rais George W Bush – alimtaja rais Trump kama muongo na kumuidhinisha Biden.

Powell anajiunga na wanachama wengine wa Republican ambao wamemuidhinisha Biden. Usiku wa kwanza wa mkutano wa chama hicho, aliyekuwa gavana wa Ohio John Kasich ni mmoja kati watu kadhaa waliojitolea kuunga mkono chama cha Democrats.

Cindy McCain, mjane wa seneta wa chama cha Republican John McCain, pia alitarajiwa kuzungumza kuhusu urafiki kati ya marehemu mume wake na Biden.

Aliyekuwa Waziri wa mambo ya nje John Kerry pia alihudhuria mkutano huo kwa njia ya video na kukosoa ungozi wa Trump.

Kerry aligusia uelewa wa Trump wa masuala ya kidunia alisema anafahamu kwamba “hakuna kinachoweza kutatuliwa bila kuunganisha taifa”.

Trump alikuwa na haraka sana ya kujibu wafuasi wenzake wa Republican wanaomkosoa na amekuwa akiendelea kumuonesha Biden kama kibaraka wa watu wa mrengo wa kushoto wenye msimamo mkali.

Sasa hivi rais yuko eneo la Arizona, alikosimama hivi karibuni akiwa katika ziara ya kampeni ya wiki moja ya majimbo muhimu sana katika kinyang’anyiro cha kuingia Ikulu ya Marekani kwa mara nyingine.

Kura nyingi za maoni zinaonesha kwamba Biden anaongoza, ingawa wiki za hivi karibuni, Trump amejitahidi kuziba pengo kati yao na uchaguzi imebaki miezi mitatu kabla ya uchaguzi mkuu wa Nchi hiyo kufanyika.