January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mapinduzi Sports klabu yapata Viongozi,Mwenyekiti ahaidi kuisuka upya klabu hiyo

Mapinduzi Sports klabu yapata viongozi
Mwenyekiti ahaidi kuisuka upya mapinduzi sports klabu 

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.

WATUMISHI wa chama cha Mapinduzi (CCM) Makao Makuu na Jumuiya zake wamepata viongozi wapya baada ya kupiga kura ya kuchagua viongozi ambao wataiongoza Mapinduzi Sports klabu.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Mapinduzi Sports Club Zakayo Kishiwi imeeleza nafasi za Viongozi waliochaguliwa kuwa ni Mwenyekiti,makamu mwenyekiti, katibu mkuu,katibu mkuu msaidizi, mweka hazina mjumbe wa mkutano mkuu na wajumbe wa kamati tendaji.

Ametaja viongozi waliochaguliwa na wajumbe katika uchaguzi huo ambao ni  Kajoro Vyohoroko kuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo,Annael Samweli Makamu mwenyekiti, na Neema Mfugale kuwa katibu Mkuu.

“Viongozi wengine waliochaguliwa ni katibu msaidizi Jumanne Mzee na Eunice Malya amechaguliwa kuwa mweka hazina.

Pia taarifa hiyo imeeleza kuwa wajumbe walimchagua Hamis Hilali kuwa mjumbe wa mkutano mkuu na kuwapitisha wajumbe wa kamati tendaji ambao ni Bushuru Mohamed, Elizabeth Muhina, na Marry Ngerangera.

Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa mwenyekiti huyo aliahidi kuifufua mapinduzi sports klabu kivingine katika
michezo yote .

“Uchaguzi wa viongozi hao ulifanyika Julai 8 mwaka huu katika ukumbi wa NEC uliopo CCM makao makuu chini ya usimamizi wa wa mwenyekiti wa uchaguzi Wilson Nkambaku,”imeeleza Taarifa hiyo.