December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mapenzi ya jinsia moja, Rais Museveni atoa msimamo wa Uganda

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameonya dhidi ya kampeni zinazounga mkono haki za wapenzi wa jinsia moja nchini humo, Mapenzi ya jinsia moja ni haramu nchini Uganda.

“Usilete upuuzi wowote hapa, Tulikuwa Washington, na wakati huu Wamarekani walipanga mkutano vizuri kwa sababu hawakuleta masuala haya. Walijikita kwenye biashara, suala ambalo ni zuri. Hawakuleta masuala yeyote kuhusu wapenzi wa jinsia moja . Lakini kama wangeleta hizo mada tungekuwa na matatizo.” Rais Museveni

Ameyasema hayo Siku ya Jumatano Rais Museven alitaja haki za wapenzi wa jinsia moja kama “upuuzi” wakati wa hotuba aliyoitoa kwenye mahafali ya Chuo cha Kitaifa cha Ulinzi.