November 12, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Maonesho ya Biashara ya Jumuia ya Afrika Mashariki yapamba moto

Na Ashura Jumapili,timesmajira,Bukoba,

Mamia ya wafanyabiashara wa nchi mbalimbali wamejitokeza katika maonesho ya Biashara ya Jumuia ya Afrika Mashariki yanayoendelea Mkoani Kagera nchini Tanzania.

Ndihohubwayo Jackson ,ametokea kikundi cha ( cooperative urumuri ) Bujumbura nchini Burundi kuja kushiriki maonesho hayo ya kibiashara Mkoani Kagera,amesema vijana wanawajibu wa kushiriki katika kazi za mikono kwa kutengeneza bidhaa za asili.

Jackson,amesema waliamua kuanzisha kikundi hicho ili cha Sanaa kwa lengo la kudumisha mila na desturi za jamii ya Afrika.

Amesema wanatumia mikono yao kutengeneza bidhaa hizo za asili kama vile vitenga kwa kutumia majani ya mgomba na wanatengeneza vikapu kwa kutumia ukili kwa ubunifu wa aina mbalimbali.

Amesema vikapu vingine vinatengenezwa kwa kutumia nyuzi za katani na vinatumika kwaajili ya kwenda kutoa mahari kwa binti aliyeposwa.

Amesema bidhaa zinazotumika kutengeneza hizo bidhaa zinapatikana kirahisi mashambani na hakuna inayotoka nje isipokuwa ni muda tu kwa vijana na wanaweza kupata kipato bila kutegemea ajira za serikali.

Ndihohubwayo Jackson ,ameshikilia kitunga kilichotengenezwa kwa nyuzi za katani anasema huwa kinatumika kwenda kutoa mahali kwa binti aliyeposwa na huwa vinatengenezwa kwa ukubwa mbalimbali

Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Toba Nguvila amesema vikwazo vinavyoweka ugumu wa kufikia soko la Afrika Mashariki viondolewe kwa wafanyabiashra kwa sababu Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suhulu Hassan ameisha fungua fursa.

‘’Tunahitaji mahusiano ya kibiashara na mzunguko wa fedha ,jumuia ya Afrika Mashariki imeboresha mfumo wa biashara taratibu zote za forodha zinafanyika mpakani’amesema Nguvila.

Amesema mamlaka zote zilizopo mpakani ziweke mabanda kwenye maonesho hayo ili waweze kutoa elimu kwa wafanyabiashara na kuendelea kupokea changamoto mbalimbali za wafanyabiashara.