Na Mwandishi wetu, Timesmajira
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade, Latifa Khamis, amesema kuwa maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba, yatafanyika kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, 2025 katika viwanja vya Julius Nyerere.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa CBE jijini Dodoma, Latifa amesema kaulimbiu ya mwaka huu ni: “Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa Sabasaba, Fahari ya Tanzania.”
Katika kuhakikisha maonesho ya mwaka huu yanafanyika kwa mafanikio, TanTrade imeandaa mikakati kadhaa ikiwemo, ukarabati wa majengo na miundombinu katika viwanja vya maonesho, ujenzi wa maeneo ya wazi kwa viwango vya kimataifa, kuimarisha usafi na huduma za afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya ya Temeke, uongeza idadi ya washiriki na wageni kwa kuandaa burudani mbalimbali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambayo italeta wasanii mbalimbali.

Aidha ameeleza kuwa lengo la maonesho hayo ni kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kukutana, kubadilishana uzoefu, kutafuta masoko pamoja na kujifunza teknolojia mpya. Aidha, maonesho haya yamekuwa pia sehemu ya kujifunza kwa wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali nchini.
Kwa upande wa wageni wa kimataifa, mabanda maalum yameandaliwa ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuongeza mapato ya fedha za kigeni. Mabanda hayo ni pamoja na, banda la Jakaya Kikwete, banda la Benjamin Mkapa, banda la Ally Hassan Mwinyi
Aidha kutakuwa na matumizi ya TEHAMA na tiketi za kuingia zitapatikana kwa njia ya mtandao kupitia mifumo ya YAS na VODACOM.
Maonesho hayo yataambatana na matukio mbalimbali muhimu, yakiwemo,Juni 26, 2025 Mapokezi ya washiriki wa ndani,Juni 27, Mapokezi ya washiriki wa nje ya nchi, Julai 3, Uzinduzi wa programu ya Urithi Wetu, ikiwalenga wanafunzi kutoka vijijini wa mikoa mitano Pwani, Mbeya, Kigoma, Zanzibar Kaskazini na Kusini, Julai 5,Made in Tanzania Day siku ya kuenzi bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini, Julai 8, Zanzibar Day, Julai 9, Siku ya Kimataifa ambapo Urusi inatarajiwa kushiriki, Julai 10, Hariana Day
Pia kutakuwa na Kliniki ya Biashara Kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali, kama TBS, Brela, n.k kwa lengo la kuweza kuwapatia huduma washiriki.
Mkurugenzi Mkuu amemalizia kwa kuwakaribisha wadau kudhamini na kushiriki kwenye maonesho haya makubwa Afrika Mashariki na Kati.
More Stories
Kapinga :Serikali inaendelea kutekeleza miradi ya umeme kwenye maeneo ya kimkakati
Vijana wa Kitanzania kupatiwa mafunzo kidijitali
TAMISA yaandaa Kongamano la Wadau wa Sekta ya Madini