Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umeendelea kutoa elimu ya Hifadhi ya Jamii kwenye Maonesho ya 10 ya Biashara ya Kimataifa ya Zanzibar yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyamanzi, Wilaya ya Magaharbi Kisiwani Unguja.
Maonesho hayo yamezinduliwa Januari 10, 2024 na Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Mwinyi, yakiwa ni sehemu ya Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Maonesho hayo ambayo yamebeba kauli mbiu isemayo “Biashara Mtandao kwa Maendeleo ya Biashara na Uwekezaji” yanawashiriki zaidi ya 500 kutoka taasisi mbalimbali za bara na visiwani, wakiwemo wajasiriamali na yanatarajiwa kufikia kilele Januari 19, 2024.
PSSSF imetumia fursa hiyo kuwahudumia wananchama wake ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu ya matumizi ya teknolojia katika kupata huduma za Mfuko, kupitia PSSSF Kiganjani.
Huduma hizo ni pamoja na kupata taarifa za Mafao yatolewayo na Mfuko, Taarifa za Michango, Taarifa za Uwekezaji ikiwa ni pamoja na Wastaafu kujihakiki.
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba (katikati) akimuhudumia mwanachama wa Mfuko huo katika banda la PSSSF kwenye Maonesho ya 10 ya Biashara ya Kimataifa ya Zanzibar, kwenye viwanja vya Nyamanzi, kisiwani Unguja Januari 14, 2024.
More Stories
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM
Watakaokwamisha mapato Kaliua kukiona cha moto
Dkt.Gwajima aagiza kuundwa kamati za ulinzi wa watoto