January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Manusura:miaka miwili ya Rais, Buzuruga yapokea zaidi ya bilioni 2

Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza

Katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia,Kata ya Buzuruga Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza imepokea zaidi ya bilioni 2, kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.

Hayo yamebainishwa na Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Diwani wa Kata ya Buzuruga Manusura Lusigaliye,wakati akiwasilisha utekelezaji wa Ilani ya chama hicho ngazi ya Kata na akizungumza na wananchi wakati akuzindua ofisi ya serikali ya mtaa wa Buzuruga Kaskazini ulienda sambamba na ugawaji wa maeneo kwa ajili ya kufanyia biashara wajasiriamali wa mtaa huo.

Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Diwani wa Kata ya Buzuruga Manusura Lusigaliye,akikata utepe kuashiria kuzindua ofisi ya serikali ya mtaa wa Buzuruga Kaskazini ulienda sambamba na ugawaji wa maeneo kwa ajili ya kufanyia biashara wajasiriamali wa mtaa huo.

Manusura ameeleza kuwa miongoni mwa miradi iliyotelelezwa kwa kipindi hicho ni pamoja na ujenzi wa shule ya sekondari ya Kata ya Buzuruga na watoto wanasoma ndani ya kata,ujenzi wa wodi ya mama na mtoto katika kituo cha afya Buzuruga chenye thamani ya zaidi ya milioni 210.

Ambapo baada ya Rais kuona tatizo katika kituo hicho upande wodi ya mama na mtoto alitoa kiasi hicho cha fedha ambao kwa sasa umekamilika kwa asilimia 100.

“Wodi ile imekamilika na wiki ijayo tunakwenda kuizindua rasmi ili wanawake wa Buzuruga waendelee kuongeza taifa kupitia wodi hiyo ,takwimu zinaonesha kituo cha Afya Buzuruga uwezo wake ni kuzalisha wajawazito 170 kwa mwezi lakini sasa inazalisha zaidi ya wanawake 900,kinazidi hadi hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Sekou-Toure,”ameeleza Manusura.

Pia wameshuhudia kituo cha daladala ustawi kimekamilika na wanawake wa pale wanapata huduma ambapo zaidi ya milioni 220 zimewekwa pale kilo.vixuri na kiwango kizuri.

“Ndani ya miaka hii miwili pekee yake Kata ya Buzuruga imepokea zaidi ya bilioni 2.2, kwa ajili ya maendeleo ya miradi mbalimbali huku kwa niaba ya halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ndani ya miaka miwili Rais ametupatia takribani bilioni 45.7 kwa ajili ya maendeleo ya miradi mbalimbali ya halmashauri hiyo,”ameeleza Manusura.

Akizungumzia ofisi hiyo ya serikali ya mtaa wa Buzuruga Kaskazini ameeleza kuwa ni ofisi ya pili kujengwa katika Kata hiyo katika miaka miwili pia wanakusudia ndani ya mwaka huu kujenga ofisi za serikali za mitaa kwa mitaa mitatu iliobaki.

Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Diwani wa Kata ya Buzuruga Manusura Lusigaliye,kushoto akiangalia kibao cha jiwe la msingi la ofisi ya serikali ya mtaa wa Buzuruga Kaskazini mara baada ya kuizindua ofisi hiyo ulienda sambamba na ugawaji wa maeneo kwa ajili ya kufanyia biashara wajasiriamali wa mtaa huo.

“Kufika Desemba mwaka huu tutakuwa tumekamilisha ofisi zote za serikali za mitaa ili wananchi waweze kuhudumia ndani ya ofisi na siyo kwingineko hii yote ni juhudi inayofanywa na CCM,”ameeleza Manusura.

Sanjari na hayo ameeleza kuwa zoezi la kuwapatia wanawake wajasiriamali ndogo eneo lamkufanyia biashara kwanza ni kwa sababu mtaa huo wa Buzuruga Kaskazini hawana genge la kununulia mahitaji yao.

“Sasa tunakuwa hapa kama genge rasmi,nawahakikishia hakuna mtu wa kuwaondoa ,zile habari za kuuzia tena barabarani hatutaki kuzisikia,za kusumbuliwa na mgambo hatutaki kuzisikia,mfanye biashara zenu kwa uhuru,”ameeleza.

Baada ya zoezi hilo hawatahitaji kuona watu wakifanya biashara barabarani na tofauti katika maeneo waliopangiwa huku lengo ikiwa ni kumuung mkono Rais ambao ameagiza kuwapanga watu sehemu husika na siyo kusambaa barabarani.

Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa ofisi ya serikali ya mtaa wa Buzuruga Kaskazini, Mtendaji wa Kata ya Buzuruga Ally Raimund, ameeleza kuwa ujenzi wa ofisi hiyo ulianza Machi 13,2022 kwa nguvu za wananchi na wadau,mpaka kufikia ukamilishaji wa boma jumla ya milioni 7.6 (7,672,000)zilitumika.

“Katika kuunga juhudi za ujenzi huo halmashauri ilitupatia kiasi cha milioni 15(15,077,075) Januari,31 mwaka huu ambapo milioni 13(13,110,500) kwa ajili ya vifaa vya ujenzi na million 1.9(1,966,575) kwa ajili ya ufundi huku katia fedha hizo kiasi cha milioni 14.6(14,679,000) na kiasi cha 398,000 ndicho kilichobaki,”ameeleza Raimund.

Kwa upande wao wananchi wa Mtaa wa Buzuruga Kaskazini akiwemo Joyce Mtondi, ameeleza kuwa mtaa wao ulikuwa hauna ofisi hivyo ametoa shukrani kwa Rais kuwajengea wodi ya mama na mtoto katika kituo cha afya cha kata yao kwani inawasaidia wanawake.

“Wanawake tunamshukuru sana kwani Kuna maeneo ambayo tumepewa kwa ajili ya kufanyia biashara ndogo ndogo tutaepukana na uuzaji wa bidhaa barabarani,”ameeleza Joyce.

Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Buzuruga Kaskazini waliojitokeza wakati wa uzinduzi wa ofisi ya serikali ya mtaa wao ulienda sambamba na ugawaji wa maeneo ya kufanyia biashara wajasiriamali wa mtaa huo.
Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Diwani wa Kata ya Buzuruga Manusura Lusigaliye, akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua ofisi ya serikali ya mtaa wa Buzuruga Kaskazini ulienda sambamba na ugawaji wa maeneo kwa ajili ya kufanyia biashara wajasiriamali wa mtaa huo.