November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Manispaa ya Iringa yafanya ziara ya kujifunza Ilemela

Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza

Viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wamefanya ziara ya kutembelea Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kwa ajili ya kujifunza namna Halmashauri hiyo inayotekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ambapo kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela wamejifunza mbinu mbalimbali za ukusanyaji wa mapato pamoja na vyanzo vyao vya ukusanyaji wa mapato hivyo Manispaa ya Iringa itaenda kuzitumia mbinu hizo.

Akizungumza Aprili 3,2024 mara baada ya kutembelea stendi ya mabasi na maegesho ya maroli Nyamh’ongolo iliopo Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela,Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada, ameeleza kuwa wamekuja mkoani Mwanza kwa sababu ipo juu katika ukusanyaji wa mapato ingawa Iringa ipo vizuri katika suala la usafi wa mazingira.

“Tunaamini kuja kuona tunaweza kufanya vizuri kwa Manispaa ya Iringa,sisi tunayo stendi ambayo ipo nje ya Mji, tunaazisha kituo kwa ajili ya malori kwaio tunaamini kuja Mwanza kujifunza tutapata kitu kizuri zaidi,”ameeleza Ngwada na kuongeza kuwa

“Hapa Ilemela mapato yapo zaidi ya bilioni 11 lakini sisi Iringa mapato yetu yalikuwa zaidi ya bilioni 4 na sasa hivi tumekusudia kukusanya bilioni 6,tunaamini kwa yale ambayo tumeyaona hapa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mapato yetu tutaenda kuyaongeza,”.


Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Godfrey Mbagali, ameeleza kuwa Iringa wanajivunia kuwa na Halmashauri safi na mwaka 2023 walikuwa wa 3 ngazi ya Manispaa.

“Tumegundua vyanzo vingine vya mapato,sisi tulikuwa hatuna chanzo cha kupakia na kushusha mizigo,pia kuna mahakama inayotembea na sisi utamaduni huu tutaenda kuanzisha kwa watu wetu ili watu wote wawe wanalipa kodi na waone kulipa kodi ni fahari, tumejifunza kuwa wale wanaozalisha taka nyingi wana kiwango chao cha kulipa ushuru vile vile wanaozalisha taka chache,kwaio tuna vitu vingi tumejifunza na wao waje kwetu wajifunze mazuri na uwekezaji tulionao na kwa sasa tunaendelea na utalii wa Nyanda za Juu Kusini,”ameeleza.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Dkt. Godfrey Mbagali, ameeleza kuwa Iringa wanajivunia kuwa na Halmashauri safi na mwaka 2023 walikuwa wa 3 ngazi ya Manispaa.

“Tumegundua vyanzo vingine vya mapato,sisi tulikuwa hatuna chanzo cha kupakia na kushusha mizigo,pia kuna mahakama inayotembea na sisi utamaduni huu tutaenda kuanzisha kwa watu wetu ili watu wote wawe wanalipa kodi na waone kulipa kodi ni fahari, tumejifunza kuwa wale wanaozalisha taka nyingi wana kiwango chao cha kulipa ushuru vile vile wanaozalisha taka chache,kwaio tuna vitu vingi tumejifunza na wao waje kwetu wajifunze mazuri na uwekezaji tulionao na kwa sasa tunaendelea na utalii wa Nyanda za Juu Kusini,”ameeleza.

Diwani wa Kata ya Mkimbizi, Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu,uchumi na Afya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Eliud Mvella, ameeleza kuwa wamejionea mambo mengi ambayo wataenda kufanyia kazi hususani wameangalia vitega uchumi vya wenzao kama stendi ya Nyamh’ongolo.

“Wenzetu walipata bilioni 20 na pointi lakini sisi ata kama tunapata fedha kidogo tunachotaka ni usimamizi wa mradi ambao unalingana na fedha tunayoipata,moja ya eneo ambalo lililokuwa linatusumbua ni upangishaji wa vibanda vya stendi,tumejifunza kwamba usimamizi ni kitu cha msingi katika shughuli yoyote ile tumeangalia maeneo ya kuegesha magari,sisi tutaenda kufanya uwekezaji huo,Ilemela siyo Jiji ni Manispaa kama tulivyo sisi lazima tukubali kuwa wenzetu wamepiga hatua tumejifunza na sisi tukawekeza kwani kuna maeneo yanafanana na kwetu,”ameeleza na kuongeza

“Tumeona wenzetu kila kitu wanatumia mashine za kieletroniki(EFD) katika kukusanya mapato na ambavyo walivyo serious ambapo abiria wakiingia stendi wanalipia na ata wenye mizigo pia, ambapo mapato yao ya mwezi na ya mwaka yanatuzidi ndio maana tumetumia fedha nyingi kuja kujifunza,”.

Diwani Viti maalumu Manispaa ya Iringa Hellen Machibya, ameeleza kuwa wameridhishwa na miradi ambayo Ilemela wanavyoiendesha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Ummy Wayayu,amezikaribisha Halmashauri nyingine kuja kujifunza Ilemela huku akieleza kuwa mkakati wao mpaka ikifika mwezi Mei Madiwani wao nao wataenda sehemu kujifunza.

“Sababu kujifunza hakuishi kila siku tunajifunza kwaio wakitua eneo wakaona vitu tofauti na hapa sehemu tunaendelea kuboresha na kuendelea na maendeleo ya Ilemela yetu,”.