Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
MWANAMITINDO Mtanzania aliyebadilika kuwa mwanaharakati wa kisiasa Mange Kimambi,ambaye kwa sasa makazi yake nchini Mrekani, amemfagilia msanii muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri hapa nchini Faustina Charles maarufu kama ‘Nandy’jinsi anavyopigana kivyake kuhakikisha mziki wake unafika mbali.
Akimpa pongezi hizo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram Mange amesema, Nandy anafaa kupigiwa Salute maana ni jeshi a mtu mmoja anayefanya vizuri sana katika tasnia ya muziki wa bongo kwa upande wa wanawake.
“Kusema kweli huyu binti inabidi apewe salute. Aisee anafanya mambo yake ya muziki bila msaada wa mtu. Ni mfano mzuri kwa wanamuziki wetu. huyu binti wa kipare anafanya mambo yake yeye mwenyewe mbele ya macho yetu.
“Aisee Nandy unatubeba mno wapare. Yani najivunia sana kwako Nandy. Huyu binti katengeneza festival yake kiutani utani tu. Sasa mpaka imedhaminiwa. Wow, bravo,” amesema Mange.
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio