Na Mwandishi Wetu, TimesMajira
MWANAMITINDO Mtanzania aliyebadilika kuwa mwanaharakati wa kisiasa ambaye kwa sasa makazi yake nchini Marekani, Mange Kimambi amemfunda msanii wa muziki wa Bongo fleva na Bosi wa Kondegang Rajabu Abdul maarufu kama ‘Harmonize’ kuachana na wanawake ambao wameshindikana na badala yake arejea kwa aliyekuwa mke wake Sarah.
Akimpa ujumbe huo kupitia Ukurasa wake wa Instagram Mange Kimambi amesema, yeye Mama yake alikuwa mmakonde wa Lindi. Kiswahili chake kilikuwa cha kimakonde kabisaa, kwa hiyo Harmonize ni Kaka yake kwa upande wa mama hivyo hana budi kumpa ushauri kama anakwenda sivyo.
“Sasa nisikilize dada yako, rudi kwa mke wako utulie. Achana na haya magume gume ya mjini. Ukikosa misabwanda unachukua siku moja moja ila tulia na mzungu mdogo wangu. Maisha yenyewe magumu uanze kukimbizana na magume gume yaliomshinda mtume utaweza?. Ona sasa wasafi wamekushinda dau mwanamke kawapa mameseji na mapicha. Ungekuwa na hela ndefu hata hiyo ya mwanae tusingekaa kuisikia huku nje. Tatizo Wasafi wamekuzidi dau la hela. We ulikuwa unawapeleka shopping mlimani City wale wamewapeleka shopping Dubai ndio maana wamekuchenjia.
“Hii ni laana ya mzungu ukae ukijua. Mzungu amekutoa mbali mno halafu unamwacha kizembe zembe lazima Mungu akunyooshe. Embu rudi kwa mke wako Tafadhali. Kajala alishapotea mjini, hakuna aliekuwa anamkumbuka hata kama yupo, wewe ndio umemrudisha kwenye trending. Kajala hana akili hata robo haoni kama anatumika tu yeye pamoja na mwanae. Haki ya nani Kajala mi nashindwa hata kumuelewa ni mama wa dizaini gani. Yani Kajala ‘single handedly’ anaharibu future ya mwanae. Yule Paula ndio atakuwa mrithi wa Wema Sepetu kwenye mascandal, mtaniambia tupo hapa.
“Halafu check DM yako huko nimekuandikia kitu. We nae sio mjanja ujue. Yani unaacha mwanamke ana hela yule unaenda kwa manungaembe yalioshindikana duniani mpaka ahera?. Yule Sarah kwao wana hela za urithi wa babake za Mengi chamtoto. Unajua ukikaa na Sarah hata mziki utaimba kama fun tu. Rudi kwa Sarah haraka sana kabla sijakubamiza, yule Sarah ataibiwa sasa hivi tena ataibiwa na hao hao wasafi shauri zako. Embu tumia akili wewe, life gumu hili, tulia kwa mzungu tafadhari. Na gari umnyang’anye umpe Sarah kama satakusamehe, Kajala akanunuliwe ingine na wasafi. Sasa ngoja nisikie ulimnunulia kwa jina lake haki ntakutukana,” amesema Mange Kimambi
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio