December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mandai: Wazee wanastaili Heshima na Usikivu wetu katika Taifa

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Kigamboni

Mjumbe wa Baraza kuu la Wazazi CCM Taifa viti 3 Bara . Ally Mandai, amesema “Wazazi wanastaili heshima na usikivu wetu mkubwa kwani Wazee ni Tunu ya Taifa letu.

Mjumbe wa Wazazi Taifa Mandai ,alisema hayo hivi karibuni Wilayani Kigamboni ambapo alisema, “Wazee ni hazina tuliyobarikiwa katika Taifa letu, ndio maana mpaka leo tunalo Taifa linaloitwa Tanzania”.

“Wazee ni watu muhimu sana katika Nchi yetu, waamefanya na wengine wanaendelea kufanya mambo mengi makubwa ndani ya Serikali na Chama chetu katika kumuunga mkono na kumsaidia Rais ws Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika Taifa letu.

Mwaka 1991 umoja wa mataifa ulipiitisha Azimio namba 46 linalozungumzia haki za wazee lakini Tanzania mwaka 2003 ikatungwa sera ya Taifa ya wazee ambapo hii ilikuwa muhimu sana kuelekea katika mabadiliko ya miongozo ya kuwahudumia wazee ikiwemo utungaji wa Sheria ya kuwahudumia Wazee.

Alisema taarifa zinaonesha kipindi cha Julai 2022 mpaka April 2023 Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum ikiongozwa na Waziri Dkt.Dorothy Gwajima imewatambua wazee zaidi ya milioni 2 katika mikoa 26 ya Tanzania.

Alisema kati ya Wazee hao milioni 2 Wazee laki 5 sawa na asilimia 25 hawajiwezi kabisa. Kufikia mwaka 2050 ongezeko la WAZEE Duniani inakadiliwa kufikia milioni 212 na Tanzania itakadiriwa kuwa na Wazee milioni 8.3 wakiwemo kati yao milioni mbili wasiojiweza kabisa.

Mandai alisema anatambua juhudi kubwa za Serikali inayoongozwa na Jemedari. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwahudumia Wazee lakini ameendelea kusisitiza jamii kutambua Uzee na Kuzeeka ni hali halisi inayohitaji uelewa wa kila mmoja na Maandalizi ili kushikamana zaidi.

Alisema Wazee ni Tunu na hadhina pamoja na kupungukiwa nguvu za mwili lakini wakiendelea kutunzwa kwa namna mbali mbali ikiwemo Huduma za Jamii wanaendelea kutupa elimu ,ujuzi ,uzoefu na kuwa sehemu ya ushauri katika maswala mbali mbali ya Nchi yetu kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu .

Aidha alisema Mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia na mmomonyoko wa maadili umefanya baadhi yetu katika Nchi zinazoendelea kuona hakuna thamani ya Wazee kwani kila kitu unaweza kutafuta katika mfumo wa TEHAMA .

Alisema anatambua nguvu kubwa ya Serikali ya CCM na Katiba ya CCM kuweka Ibara ya Mabaraza ya Wazee na kuyaanzisha, CCM ni kimbilio sahihi la Wazee pia inajidhihirisha na kazi njema na bora inayoendelea kufanywa na Mwenezi wa CCM Taifa Paul Makonda kwa kuonesha dhahiri kuwa CCM ndiyo sikio na mdomo wa Watanzania .

Alitumia fursa hiyo pia kumpongeza sana Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Samia Suluhu Hassan, Kamati Kuu na Halmashauri kuu ya CCM Taifa kwa kumteua kwa sauti moja Paul Makonda kwani amekuwa mstari wa mbele katika Chama kusikiliza kero za watu wote wakiwemo Wazee. Tuendelee kuwapongeza
Viongozi wote, kuwaunga mkono kwa maslahi mapana ya Taifa letu bila kusahau kila mmoja afanye wajibu wake.