January 15, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Man United kuwania saini ya Camavinga

MANCHESTER, England

KLABU ya Manchester United ipo katika jaribio la kumsajili kiungo wa Kimataifa wa Ufaransa, Eduardo Camavinga kutoka Rennes.

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 18, alicheza mechi tatu kwenye Mashindano ya Ulaya U-21.Huku Rennes wako tayari kumuuza Camavinga takribani euro milioni 30 (Pauni 25.7m) kwa kile wanachodai wanaweza kumpoteza bure msimu wa majira ya joto, wakati mkataba wake utakapomalizika.

Hata hivyo, mchezaji huyo amekuwa chaguo la muda mrefu kwa United na vilabu vingine, haswa Paris Saint-Germain, pia wanavutiwa nae.

Mnamo Agosti 2020, Camavinga aliitwa kucheza kwenye timu ya wakubwa ya Ufaransa baada ya Paul Pogba kukutwa na COVID-19. Katika kipindi hicho, alikua mchezaji mdogo zaidi kuitwa katika timu ya wakubwa ya Ufaransa tangu René Gérard mnamo 1932, ambaye alikuwa na umri wa miaka 17, miezi tisa na siku 17.