Na Mwandishi Wetu , Timesmajira Online
KAMPENI ya ‘Magift ya Mixx Pesa’ inaendelea kunogesha msimu huu wa mwisho wa mwaka kwa kuendelea kumwaga mamilioni ya shilingi kwa watanzania kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.
Hadi sasa, kampeni hiyo imeendelea kuwatoa washindi wa kila siku na wiki, ikiwa ni dhamira ya Mixx by Yas kuwazawadia wateja wake, kuthamini uaminifu wao na kuhamasisha matumizi ya huduma za kifedha kidijitali.

Katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi 10 wapya, Meneja wa Wateja Maalum wa Mixx, Mary Rutta alisema kampeni hiyo imekuwa kivutio kikubwa kwa watumiaji kutokana na urahisi wa kushiriki na uhalisia wa zawadi zinazotolewa.
Akizungumza na wanahabari, Rutta amesema kampeni ya Magift ya Mixx Pesa imekuwa na mafanikio kwani wameendelea kuleta tabasamu katika nyuso za wateja wao na wanajivunia kuendelea kuwathamini kwa kuwapa zawadi kila wiki.

“Mpaka sasa tumeshatoa zawadi zaidi ya washindi 25, na leo tunakabidhi zawadi kwa washindi 10.
“Washindi wetu wa wiki hii wanatoka katika mikoa tofauti ikiwemo;- Mara, Dodoma, Morogoro, Dar es Salaam na visiwani Zanzibar,” almesema.
Amesema, washindi wa kampeni hiyo hupatikana kupitia miamala ya kawaida wanayofanya kila siku, ikiwemo kuweka au kutoa pesa, kupokea fedha kutoka benki, kutumia huduma ya Lipa kwa Simu, kuchukua mikopo, kununua vifurushi, au kupakua Mixx Super App.

Kampeni hiyo sasa inaingia katika hatua yake ya mwisho, huku leo ikisubiriwa droo kubwa ya kupata washindi wa Tsh 1,000,000 kila siku pamoja na kutafuta mshindi mmoja wa Tsh 10,000,000, ambaye ataingia mwaka mpya akiwa na mafanikio makubwa kupitia zawadi hiyo.
“Tunamuita mshindi huyu ‘Mixxionea’. Tunawahimiza wateja waendelee kufanya miamala kwa wingi ili kujiongezea nafasi ya kushinda zawadi zilizobaki,” ameongeza Rutta.
Kwa upande wake, mmoja wa washindi wa milioni moja wa wiki hii, Jenipher Elisha Sungwa wa Mbezi Kimara, aliipongeza Mixx kwa kuanzisha kampeni yenye manufaa halisi kwa wananchi.“Nawashukuru sana Mixx kwa kampeni hii.

Fedha nilizoshinda nitazitumia kuongeza mtaji wa biashara yangu ya saluni. Ni jambo la kutia moyo kuona kampuni za kifedha zinawagusa wananchi moja kwa moja,” amesema.
Kampeni ya “Magift ya Mixx Pesa” inaendelea kote nchini, na watumiaji wa huduma mbalimbali za Mixx wanayo nafasi ya kushinda kila siku hadi kampeni itakapofikia tamati januari 04, 2025.

More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina