December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mamia wamzika Bi Hindu

Na Mwandishi wetu,timesmajira, Online

Mamia ya wananchi, viongozi, wanamichezo, wasanii wa tasnia mbali mbali nchini Jumapili 10 Julai 2022 wamejumuika katika mazishi ya Msanii Nguli wa Filamu Chuma Suleiman Maarufu (Bi Hindu) yaliyofanyima nyumbani kwake Magomeni Butiama na kuzikwa katika makaburi ya Mwinyi Mkuu Jijini Dar es Salam

Chama cha Mapinduzi kitamkumbuka Bi Chuma kwa mchango wake mkubwa katika kutetea utaifa wetu kwa kudumisha utamaduni, mila, silka na desturi zetu hasa katika kuelimisha, kuhamasisha, kuburudisha na kulea rika zote kupitia semi, tungo na ujumbe maridhiwa katika nyakati tofauti” Sehemu ya salam za pole zilizowasilishwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka.

Pamoja na viongozi kadhaa walitoa salamu za pole ni Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa aliwasilisha salamu za Serikali na mkono wa rambi rambi kutoka kwa Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Samia Suluhu Hassan

Chuma Suleiman( Bi Hindu) alifariki dunia Jumamosi Julai 9,2022 baada ya kuugua kwa muda mrefu.