January 3, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mambo yanayosababisha ugumba kwa wanawake

UGUMBA ni tatizo ambalo limekuwa likiikumba jamii zetu mbalimbali kwa muda mrefu sana, na kwa kiasi kikubwa wanawake wamekuwa wakitupiwa lawama kuwa wao ndio sababu ya kukosa mtoto!.

Ukweli ni kwamba tatizo hili la ugumba linaweza kusababishwa na mwanaume au mwanamke. Miaka ya hapa karibuni taizo hili limekuwa likiongezeka zaidi sehemu mbalimbali duniani ikiwemo na hapa nchini.

Tafiti zinaonesha asilimia 12 mpaka 28 ya wenzi duniani wanakadiriwa kuwa na tatizo la ugumba ambapo kumekuwa na njia mbalimbali za kutibu tatizo hili na kusaidia watu wengi.

Ugumba ni hali ya kutoweza kupata ujauzito kwa kipindi cha mwaka mmoja au zaidi kwa wenzi ambao wamekuwa wakifanya wenzi bila kutumia njia zozote za uzazi wa mpango.

Wanawake ambao wanaweza kupata ujauzito lakini hawawezi kukaa naujauzito pia wanaweza kuwa wagumba.Ugumba wa kike na utasa wa kiume huathiri mamilioni ya watu duniani.

Mimba ni matokeo ya mchakato ambao una hatua nyingi. Ili kupata ujauzito mwili        wa mwanamke lazima utoe yai kutoka kwa moja ya ovari (ovulation), Yai  lazima lipitie mrija wa fallopian kuelekea kwenye uterasi (mfuko wa uzazi), Manii lazima ijiunge na (yai lililorutubishwa) njiani, Yai  lililorutubishwa lazima lishikamane ndani ya uterasi (kupandikiza).Ugumba unaweza kutokea ikiwa kuna shida yoyote kwenye hatua hizi.

JE UGUMBA NI TATIZO LA MWANAMKE TU?

Ugumba sio shida ya wanawake tuu. Wanawake na wanaume wanaweza kuwa na shida ambazo husababisha utasa /ugumba.

Karibu theluthi moja ya visa vya ugumba husababishwa na shida za wanawake ,theluthi nyingine ya shida ya utasa ni kwa sababu ya mwanamume. Kesi zingine husababishwa na mchanganyiko wa shida za kiume na za kike au na shida zisizojulikana.

NINI HUSABABISHA UGUMBA KWA WANAWAKE

Sababu kuu ya ugumba inahusisha matatizo ya yai kupevushwa, kuharibika mirija ya uzazi ( falopian tube ) au mfuko wa uzazi (uteras), au matatizo ya mlango wa uzazi(cervix). Vitu vingi vinaweza kubadilisha uwezo wa mwanamke kupata mtoto. Hii ni pamoja na:

UMRI

Umri unaweza changia pia, kadri mwanamke anavyokua kiumri ndivyo uwezo wake wa kupata ujauzito unapungua. Kuzeeka hupunguza nafasi ya mwanamke kupata mtoto kwa njia zifuatazo:

Ovari zake huwa na uwezo mdogo wa kutoa mayai, ana idadi ndogo ya mayai iliyobaki mayai yake hayana afya. Ana uwezekano mkubwa wa kuwa na hali ya kiafya ambayo inaweza kusababisha shida za uzazi
 

UVUTAJI SIGARA

Uvutaji wa sigara unahusishwa na matatizo kama mirija ya uzazi (fallopian tube)  kuziba (kuzuia yai na manii kukutana) na hatari kubwa ya ujauzito wa ectopic ( mimba kutunga nje ya uzazi)

MATUMIZI YA POMBE KUPITA KIASI

Ingawa haijulikani haswa jinsi pombe inavyoathiri uzazi kwa wanawake, utafiti unaonyesha kuwa hata kunywa pombe kidogo kunaweza kuchelewesha wakati wa kupata ujauzito, na kupunguza uwezekano wa kupata mtoto mwenye afya.

Wanawake ambao hunywa pombe nyingi (vinywaji saba au zaidi kwa wiki au zaidi ya vinywaji vitatu kwa tukio moja) wana uwezekano mkubwa wa kuwa na shida ya kuzaa.

Pombe pia inaweza kuathiri ovulation, ambayo inaweza kufanya iwe ngumu kushika mimba.

MAWAZO

Wakati mawazo peke yake hayaonekani kusababisha utasa au ugumba, mafadhaiko/ mawazo yanaweza kusukuma wanawake kuelekea kwenye tabia mbaya ambazo zinaweza kuathiri kuzaa kwao.

Kwa mfano, unapofadhaika, unaweza kulala kupita kiasi au kulala kidogo, kula chakula bila mpangilio au kukosa hamu kabisa yakula,

kukosa  muda wa kutosha wa kufanya mazoezi au kujisukuma kufanya mazoezi magumu sana, kunywa  pombe nyingi, kuvuta  sigara, kunywa  kahawa nyingi, kupoteza hamu ya kushiriki tendo la ndoa.

Sababu hizo zote zinaweza kuchangia kuathiri upatikanaji wa mimba na kuwa mgumba. Hivyo kwa ushauri na matibabu wasiliana na DR.Mwaka ,daktari bingwa wa uzazi.

Utakumbana na matatizo kama hali ya kutokwa damu isiyo ya kawaida, maumivu ya tumbo la uzazi, homa, kutokwa uchafu usio wa kawaida sehemu za siri, maumivu wakati wa kujamiana, kuvimba au kuwasha sehemu za siri.

Kwa ushauri, matibabu tembelea MWAKA INTERNATIONAL

UBUNGO PLAZA, GHOROFA LA PILI AU PIGA SIMU KWA NAMBA: 0785 100 100 AU 0758 100 100