December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mamba waua kwa nyakati tofauti Sengerema

Judith Ferdinand, Mwanza 

Watu wawili wamefariki baada ya kuliwa na mamba kwa nyakati tofauti katika Ziwa Victoria wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

Akizungumzia tukio hilo  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza SACP.Wilbrod  Mutafungwa, ameeleza katika  tukio liliilotokea Machi 24,2023 majira ya saa  1(19:00) jioni huko mwalo wa Kazunzu, kijiji na Kata ya Kazunzu, katika fukwe za ziwa Victoria kuliripotiwa taarifa ya mtu kuliwa mamba. 

Baada ya taarifa hiyo Askari Polisi kwa kushirikiana na wananchi walifika eneo hilo ambapo ndugu waliweza kuutambua mwili wa mtu aliyekamatwa na kuliwa na mamba kuwa ni Salome Dotto  mwenyewe umri wa miaka 30,mkazi wa Kazunzu.

Ambapo Kamanda huyo ameeleza kuwa mwili huo umefanyiwa uchunguzi naa daktari na tayari umekabidhiwa kwa ndugu kwa taratibu za mazishi.

Huku tukio jingine liliilotokea Machi 9,2023 majira ya   saa 7 (13:00) huko kijiji cha Izindabo, kata na tarafa ya Buchosa Wilaya ya sengerema, kuliripotiwa taarifa ya mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Primitiva Evarist  mwenyewe umri wa miaka 56, mkazi wa Izindabo.

Mtu huyo alifariki baada ya kukamatwa na kuliwa na  mamba wakati akinawa miguu katika fukwe za ziwa victoria.

Ambapo mwili wa Primitiva Evarist ulitambuliwa na ndugu na kufanyiwa uchunguzi kisha kukabidhiwa kwa taratibu za mazishi.

Jeshi hilo limwaasa wananchi hususani wanaofanya shughuli zao katika fukwe za Ziwa Victoria kuchukua tahadhari ya usalama wao wenyewe ili kujiepusha na madhara yanayoweza kujitokeza.