November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mama wa watoto waliofanyiwa ukatili aomba msaada

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online

MKAZI wa Kata Kivule Majohe, Wivina Alkadi(35) ambaye watoto wake wawili walifanyiwa ukatili na Mume wake kwa kulawitiwa na mwingine
kumpa ujauzito na kufungwa miaka 60, ameiomba jamii, Serikali na watanzania kumsaidia huduma muhimu za kujikumu kimaisha.

Wivina ametoa ombi hilo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari
wakati wadau wa kupinga ukatili wa Kijinsia kutoka nchini Ethiopia walipotembelea kituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Majoye (KC MAJOHE)kwa lengo la kujifunza.

Amesema amekuwa akiishi maisha magumu ambayo yamekuwa yakisababisha kushidwa kuhudumia familia yake.

“Nina watoto watano na mjukuu mmoja tumekuwa tukiishi maisha magumu kula kwetu kwa tabu, kukaa pia kwa shida nimelipa kodi ya miezi sita inatarajia kuisha mwezi wa nne hadi sasa sijajua kodi napata wapi naomba Serikali na watanzania kwa ujumla mnisaidie, “amesema huku akilia.

Wivina amesema kutokana na ugumu huo wa maisha amekuwa akijishughulisha na biashara ndogo ndogo ya uuzaji maandazi lakini imekuwa akikidhi mahitaji.

Wivina amesema anachoomba zaidi ni kupata sehemu ya kuishi kwasababu sasa amekuwa akiiangaika ni wapi atapata fedha kwa ajili ya kulipa kodi.

Aidha Wivina alikishukuru Kituo cha maarifa na Taarifa Kata ya Majohe (KC MAJOHE )kwa kuwa nae bega bega kabla ya hukumu na baada ya hukumu.

Amesema kituo hicho kimekuwa kikimpatia msaada mbalimbali ikiwemo kumpatia godoro la kulalia pamoja na kumchukua binti yake aliyepewa ujauzito na muwe elimu ya mafunzo ya chereani.

Kwa upande wake Mwanachama wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Rehema Mwateba, amesema kuwa wakati umefika wa kuzungumza ukweli kuhusu ukatili unaofanyika.

“Jamii inatakiwa kukemea vikali vitendo vya ukatili vinavyofanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waadilifu jambo ambalo linapelelea kuongezeka kwa mmong’onyoko wa madiili na kuacha baadhi ya familia kukosa malezi na kuwa tegemezi,”amesema

Aidha Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Majohe(KC MAJOHE )Tabu Ally, alisema ni muhimu kuwachukulia hatua za kisheria wahusika wa matukio ya kiukatili.

Amesema katika Kata hiyo , kumekuwa kukijitokeza matukio mengi ya ukatili wa kijinsia huku jamii ikiwa bado na uelewa mdogo wa kuripoti matukio hayo.

“Bado jamii inauelewa mdogo juu ya masuala ya ukatili wa kijinsia..lakini kupitia kituo chetu tumekuwa tukitoa elimu pamoja msaada mwa wahanga kwa kuhakikisha wanafika sehemu husika pamoja na wahusika kuchukuliwa hatua,”amesemaTabu.

Kwa upande wake wadau wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia kutoka nchini Ethiopia, Rediet Asfew wamesema kuwa wataendelea kutoa ushirikiano na TNGP katika kufanya uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake.

Wivina Alkadi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu chagamoto mbalimbali anazopitia