February 25, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mama Samia Legal Aid Campaign yawa mkombozi kwa wananchi Mbeya

Na Esther Macha TimesmajiraOnline,Mbeya

MKUU wa Mkoa wa Mbeya,Juma Homera amesema kuwa mpango wa msaada wa kisheria wa Mama Samia Legal Aid umerudisha furaha kwa wananchi kutokana na malalamiko na kesi nyingi kushughulikiwa kwa wakati na  weledi mkubwa.

Amesema kuwa ujio wa msaada huo wa kisheria kwa mkoa wa Mbeya umeleta matokeo makubwa hususani kwenye malalamiko ya migogoro ya ardhi  pamoja na ukatili wa kijinsia .

Homera amesema hayo February 24,2025 wakati wa ufunguzi  wa Samia Legal Aid Campaign  ambayo imefanyika  katika viwanja vya Stendi ya Kabwe Jijini Mbeya na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na viongozi wa dini na kimila.

“Tumeona matokeo yake na mmeona jinsi wananchi walivyojitokeza kwa wingi  hapa watu Wana matatizo,  ndo maana yake jambo hili ni muhimu na  mtambuka kwa wananchi wa Jiji la Mbeya  hivyo tumpongeze Rais Samia kwa ubunifu huu mkubwa alioanzisha wa mama Samia legal campaign kwani kesi nyingi zinashughulikiwa na  wizara ya katiba na Sheria inatimiza wajibu wake vizuri “amesema Mkuu wa mkoa wa Mbeya

Hata hivyo Homera amesema kuwa utekelezaji wa Kampeni ya msaada wa kisheria ngazi ya mkoa ilizinduliwa Jijini Dodoma April 25 ,2024  na Waziri mkuu Kasimu Majaliwa na kutoa siku 10,kusikiliza malalamiko ya wananchi na matokeo yake yanaonekana na hali ilivyo kwasasa mabadiliko ni makubwa kwa jinsi kesi zinazovyosikilizwa.

Aidha Homera amesema dhumuni kuu la msaada wa kisheria ni kuongeza uelewa wa kisheria kwa wananchi ,kuimalisha huduma ya kisheria kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia,wanaume wenye shida mbali mbali, kutoa elimu ya usimamizi wa mirathi,utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala.

Kwa upande wake Mwakilishi wa TLS  Kanda ya Mbeya,Baraka Mbwilo amesema kuwa  mkoa wa Mbeya una migogoro mingi ya ardhi ambayo inatokana na sababu mbali mbali ikiwemo mwingiliano wa shughuli za kiuchumi,uzembe kwa baadhi ya watendaji wa serikali kutozingatia majukumu yao ipasavyo.

Aidha amesema pia migogoro mingine ni pamoja na mirathi ambapo wanawake hunyanyaswa na ndugu wa mume wakidhani mali zilizochumwa na marehemu ni mali yao lakini sio mali za mjane na watoto.

Faraja Nchimbi ni mjumbe wa bosi wa kitaifa ya msaada wa kisheria amesema kuwa pia kuna changamoto ya uelewa mdogo kwa makundi maalum kwa watendaji wa serikali ngazi za chini hususani ngazi za vijiji na hivyo kupelekea kutoa uamuzi unaoweza kuathiri pamoja na uwepo na Mila na desturi zilizopita na wakati.

“Ushauri wa bodi ipo haja wizara  ya katiba na Sheria kuimarisha ukaguzi kwa mashirika yanayotoa huduma ngazi ya jamii ili kujiridhisha na huduma zinatolewa kwa jamii nalisema hili sababu bodi imebaini kuwa uwepo wa mashirika ya wasaidizi wa kisheria wanaotoa huduma bila kufuata matakwa ya kisheria ikiwemo kutoa huduma hizo bila kujisajili “amesema Nchimbi .