April 16, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mama ongea na Mwanao kushiriki tamasha la Mtoko wa Pasaka

Na Bakari Lulela, Timesmajira Online,Dar

TAASISI ya Mama Ongea na Mwanao, inatarajia kushiriki kwenye tamasha la Mtoko wa Pasaka,litakalofanyika Aprili 20,2025,jijini Dar-es-Salaam.

Akizungumza jijini hapa Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Steve Nyerere amesema tamasha hilo,litakuwa la kipekee kwa waumini wa dini ya Kikristo na Watanzania kwa ujumla, ambapo kauli mbiu itakuwa isemayo ‘kwa maombi tutashinda’.

Amesema kutakuwa na waimbaji mahili wa nyimbo za injili akiwemo mwimbaji maarufu Christina Shushu na waimbaji wengine kutoka nchini hapa na nje ya mipaka ya Tanzania.

“Mama ongea na mwanao tutashiriki kwa pamoja katika tamasha hilo, jukumu kubwa litakuwa ni kumuombea Rais wetu kuweza kushinda katika uchaguzi mkuu 2025,” amesema Steve.

Kwa upande wake muimbaji maarufu wa nyimbo za injili Christina Shushu amesema siku hiyo itakuwa ya aina yake ambapo wanamuziki wa nyimbo za injili na kwaya wataonesha umahiri wao.

Hata hivyo katika tamasha Hilo kutakuwa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo Kenya na Uganda.