January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mama Lishe 100 Mbeya kupatiwa mitaji

Na Esther Macha,TimesmajiraOnline, Mbeya

MJUMBE wa Halmashauri ya Kuu Taifa CCM (MNEC)Ndele Mwaselela amehaidi kuwawezesha mitaji Mama Ntilie 100 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya katika Mji mdogo wa Mbalizi bila kujali itikadi za vyama ili waweze kufanya shughuli mbalimbali za uzalishali mali.

Mwaselela amesema hayo Mei,26 2024 wakati akizungumza na vijana wa makundi mbalimbali katika Halmashauri ya wilaya ya Mbeya ambao aliwaandalia chakula cha jioni lengo likiwa ni kujadili changamoto zinazoyakabili makundi hayo.

MNEC Ndele Mwaselela

Aidha Mwaselela amesema anataka kuona Mama Ntilie ambao wana sura ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan wakiwa na tabasamu la kutosha kutokana na kuwa vizuri kiuchumi na kuongeza thamani ya maisha yao.

“Tuikimbize Mbeya vijijini yetu na asiwepo wa kuzuia hili jambo tunahitaji kusonga mbele ndo sababu hapa nimeita vijana wa makundi yote kutoka kata zote bila kuangalia itikadi za vyama vyao kikubwa ninachotaka tuungane kwa pamoja ili Wilaya ya Mbeya iweze kupaa kiuchumi na vijana waweze kupaa kiuchumi,”amesema Mwaselela.

Kenny Laulesi ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu wa Taifa Mkoa wa Mbeya amesema kwamba hafla hiyo itatengeneza umoja wa kuweza kujua mipango ya wana Mbeya vijijini kwa kile wanachotaka .

“Ameamua kwa dhati kufanya kazi ya Chama Cha Mapinduzi lakini kufanya kazi ya kwake peke yake ,ili kuweza kutengeneza maendeleo ya Mkoa wa Mbeya,anachokifanya ni kuagizwa na Rais Dkt. Samia kukaa na makundi ya vijana ,wazee na watoto kwa ajili ya kutengeneza mustakabali wa Mbeya Vijijini na Mkoa wa Mbeya pamoja na taifa kwa ujumla,”amesema Laulesi.

Baadhi ya vijana walioshiriki chakula cha jioni na Mwaselela