January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mama aliyeua watoto wake wawili kwa kuwanywesha sumu afariki

Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya

MAMA mzazi wa watoto wawili walionyweshwa sumu aitwaye Daines Mwashambo ((30)mkazi wa Kijiji cha Mashese kata ya Ilungu wilaya ya Mbeya aliyekuwa anaendelea na matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya amefariki dunia wakati akiendelea na matibabu.

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema mama huyo alifariki March 9 mwaka huh majira ya saa 10.15 jioni katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya.

Kamanda Kuzaga amesema kuwa March 5 mwaka huu mtuhumiwa Dainess akiwa nyumbani kwake Kijiji cha Mashese kata ya Ilungu aliwanywesha sumu ya kuulia magugu aina ya “Pare Force” watoto wake wawili na kusababisha vifo vya watoto hao

Amesema kuwa baada ya kutekeleza tukio hilo la kuwanywesha sumu watoto wake mtuhumiwa nae alikunywa sumu hiyo iliyopelekea kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya kwa matibabu.

Aidha Kamanda Kuzaga amesema mtuhumiwa aliendelea kupatiwa matibabu Hospitalini hapo lakini alifariki duniani.March 9 mwaka huu.