Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Makumbusho ya Taifa imetakiwa kuangalia na kutumia njia bora za uhifadhi wa urithi wa asoli na utaduni ili kuendelea kuhifadhi urithi adhimu wa historia ya nchi yetu kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
Wito huo umetolewa na Dkt Edwinus Chrisantus Lyaya Mhadhiri wa Urithi na Akiolojia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa Maadhimisho ya siku ya Zinjanthropus Boisei yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es Salaam.
Lengo la maadhimiaho haya ni kujenga uelewa kwa wananchi juu ya chimbukonla mwanadamu ambapo mwanadamu wa kale alivumbuliwa na Dr Mary Leakey tarehe 17 Julai 1959 katika bonde la Olduvai Gorge, Wilaya ya Ngorongoro.
Dkt Edwinus Chrisantus ameipongeza Makumbusho ya Taifa kwa kuona umuhimu wa kuendelea kufanya utafiti na kuendelea kuhifadhi mikusanyo ya mabaki ya kumbukumbu za historia ya Nchi yetu sambamba na kuutangaza kupitia program zinazo shirikisha jamii kama vile matamasha ,maadhimisho na maonesho.
Akizungumzia Maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw. Achilles Bufure amesema huu ni mwaka wa tatu kufanya Maadhimisho haya ya Zinjanthropus Boisei tangu kugundulika kwake mwaka 1959 na kwamba maadhimisho haya yanalenga katika kuelimisha jamii mawanda mapana ya ufahamu juu ya umuhimu wa urithi huo adhimu tuliobalikiwa nao hapa Tanzania.
“Leo tumeona wanafunzi walioshiriki maadhimisho haya wakitumia zana mbalimbali zikiwemo zana za mawe kukatia nyama, mikuki na mishare iliyotumiwa kuwindia wanyama enzi za maisha ya mwanadam wa kwanza sambamba na kujifunza namna ya njia zinazotumiwa na watafiti wetu wanapoenda maeneo husika.”alisema Bw. Achilles Bufure
Kwa upande wake Vitalis Obonyo Mwanafunzi wa Chuo cha Agakhani alieleza kuwa wamefarijika sana kushiriki maadhimisho haya ya siku ya kumbukumbu ya kugunduliwa fuvu la mwadamu wa kale ambayo imetupa fursa ya kujionea kwa macho mabaki ya kumbukumbu za historia ya fuvu la mwadamu wa kale na mabaki mengine mengi tumeona tulipotembelea kumbi zenye mikusanyo hapa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni.
Wanafunzi hao walioshiriki maadhimisho haya ya siku ya Zinjanthropus Boisei wamesema kuwa wamefurahia sana kutumia zana za mawe kukata nyama na wamefahamu kuwa Zinjanthropus Boisei siyo mwanadam wa kwanza kuishi bali ni Fuvu la mwanadamu wa kwanza kugunduliwa. Ila mwanadamu wa kwanza tumefahamu kuwa amegunduliwa Chad – Sahelanthropus tchadensis aliishi miaka million 7, Australopithecus Afarensis aliishi miaka 3.8 million akifatiwa na Zinjanthropus Boisei aliyeishi miaka 2.5million.
Aidha kwa upande wake Mhifadhi wa Paleontology Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni ambaye ni mratibu wa Maadhimisho hayo Bw. Wilson Jilala amewashukuru Wanafunzi mbalimbali walioshiriki kutoka shule ya Msingi Bunge, Shule ya Msingi Bamba, Shule ya Sekondari Kisutu,Chuo cha Agakhani na Wataalam mbalimbali kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam.
“Jamii inatakiwa kutembelea Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni ili kujifunza na kujionea kwa macho urithi na Utamaduni wetu tuliobarikiwa ,siyo tu kujifunza watapata burudani pia watakapotembelea maeneo haya yaliyohifadhi historia ya urithi wetu” Alisema Bw. Wilson Jilala.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa