Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Cham Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda amemkabidhi Mwanamama mkazi wa Iringa, mchoro wake wa eneo lake analolimiliki ikiwa ni miaka 4 imepita tangu kufuatalia haki yake hiyo.
Mwanamama huyo jana tarehe 8 Februari, 2024 alitoa kero yake hiyo kwa Mwenezi Makonda mbele ya kadamnasi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Iringa Mjini ambapo alisema alishalipa fedha za kwaajili ya kupatiwa mchoro wa eneo lake lakini hadi sasa ni miaka 4 imepita hajapatiwa mchoro huo na ameshafika kutoa taarifa katika ofisi zote hadi kwa Mkuu wa Wilaya.
Mara baada ya kusikia kero hiyo, ndipo Mwenezi Makonda aliagiza Ofisi ya Mkurugenzi kushughulika jambo hilo ndani ya siku moja ilikusudi Mwanama huyo kupatiwa mchoro wake na kuahidi kulifuatilia jambo hilo kabla ya kutola mkoani Iringa.
Hatimaye mapema asubuhi ya leo agizo hilo limetekelezwa na Mwenezi Makonda akamkabidhi mchoro Mwanamama huyo.
More Stories
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini
Kampeni msaada wa kisheria ya mama Samia kutatua kero za kisheria Katavi
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25