November 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makocha wa India kuinoa timu ya Taifa ya Kabaddi

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MAKOCHA wa kimataifa wa mchezo wa Kabaddi kutoka nchini India, Amrik Singh na Vijender Singh wanatarajiwa kutua hapa nchini kwa ajili ya kuanza kuinoa timu za Taifa ya Tanzania ya mchezo wa Kabaddi za wanawake na wanaume zinazotarajia kuingia kambini Novemba Mosi.

Makocha hao ambao wameteuliwa na Bodi ya mchezo wa Kabaddi ya Dunia watasaidiana watafanya kazi kwa kusaidiana na kamati maalumu ikiwa ni pamoja na Kamati ya
ufundi kuelekea mwenye mashindano ya Kabaddi ya Afrika yatakayofanyika Desemba 11 hadi 13 hapa nchini.

Katika mashindano hayo ya Afrika, Tanzania itawakilishwa na timu ya wanaume na wanawake pia zipo timu kutoka nchini Kenya, Cameroon, Egypt, Mauritius, Sirra Leone, Uganda, Afrika Kusini, Nigeria na Zimbabwe.

Lakini timu za Uingereza, Malaysia, Taiwan, Iraq na India zikionesha nia ya kuja kama waalikwa ingawa ushiriki wao utategemea maamuzi ya bodi ya Kabaddi Afrika (Africa Kabaddi Federation na World Kabaddi).

Tayari kamati hiyo imeshatangaza vikosi hivyo vya timu za Taifa ambapo kila kimoja kinaundwa na wachezaji 20 kutoka Mikoa mbalimbali ya Taanzania Bara na Visiwani.

Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa Kabaddi Tanzania (TKSA), Abbdallah Nyoni ameuambia Mtandao huu kuwa, kama kila kitu walichopanga kitakaa sawa, basi vikosi hivyo vitaingia kambini Novemba Mosi.

Wachezaji hao 40 waliochaguliwa watapewa mafunzo na makocha Amrik na Vijender ambao wameteuliwa na Bodi ya Kabaddi ya Dunia ambao watashirikiana kikamilifu na makocha wa hapa nchini kutipia kamati ya Ufundi.

Amesema kuwa, pia ndani ya mwezi Novemba, Kamati Maalum itafanya tathimini ya maandalizi ya Mashindano ya Afrika ikiwa ni pamoja na kuandaa miundombinu ya mashindano (hotel kwa timu,viwanja,chakula na usafiri pamoja na mambo mengine muhimu ikiwemo semina elekezi kwa vyombo vya habari.

“Baada ya kukamilika kwa mambo haya muhimu, Desemba 8 na 9, 2020 tutapokea timu ya wakaguzi na maafisa wa ufundi pamoja na wanahabari toka nje watakaoambatana na maofisa wakuu wa World Kabaddi, Africa Kabaddi Federation na NKIF na Desemba 10 timu zitaanza kuwasili kwa ajili ya mashindano yatakayoanza tarehe 11 hadi 13,” alisema kiongozi huyo.

Kuelekea mashindano hayo kikosi cha timu ya Taifa ya wanawake kinaundwa na Zuhura Ally, Nsara Mkima, Mwanahamisi Said, Agnes Alfan, Zuwena Hassan, Jane Fungo, Mezea Abdallah, Sauda Moshi, Marry Kidimwa, Happiness Mikanili, Janet Bujiku, Upendo Yunus, Aziza Juma, Zaitun Abdallah, Aneth Mosha, Christina Moshi, Ruce Sechonge, Zena Msangila, Nasra Makowa na Rocemary John.

Kwa upande wa wanaume kikosi chao kina oland Aswile, Best Mpanda, Joseph Mkinga, Musa Mustafa, Said Tindwa, Juma Sultan, Abdul Ally, Hassan Ally, Shija Bujiku, Shigela Magobo, Masanja Mtemi, Athumani James, Manase Madusa, Hussein Mbembati, Mahamudu Mahamudu, Godfrey Ngalu na Peter Asangwise.