Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online,Mwanza
Viongozi , wataalamu na wananchi kila mmoja kwa nafasi yake wametakiwa kuhakikisha wananusuru fumwe zilizopo nchini, huku wafanyabiashara,wadau na sekta binafsi kuchangamkia fursa ya kuwekeza katika fukwe kwa kutoa huduma pamoja na ajira.
Agizo hilo limetolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango wakati akifungua jukwaa la maendeleo endelevu (GGP), lililoandaliwa na Taasisi ya Uongozi ili kujadili usimamizi madhubuti wa fukwe kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini linalofanyika kwa siku mbili (Novemba 23-24,2022) jijini Mwanza.
Dkt.Mpango ameeleza kuwa Tanzania imebarikiwa na Mungu kwa kuzungukwa na maji maeneo ya nchi na kuwa na fukwe za kuvutia kwa baadhi ya mikoa.
“Bado hatujaweza kutumia kikamilifu fukwe hizi kwa ajili ya maendeleo kama ilivyo katika nchi nyingine asilimia kubwa za fukwe zetu hazijaendelezwa zinakabiliwa na tatizo la uharibifu wa mazingira unaotokana na ongezeko la shughuli za binadamu kandokando ya fukwe ikiwemo uchimbaji wa mchanga , utupaji taka ovyo ikiwemo taka maji na taka ngumu ,ujenzi holela ,uvuvi haramu kilimo na ufugaji holela,”ameeleza Dkt Mpango.
Ameeleza kuwa athari hizo zinaonekana zaidi kando kando ya mito na kwenye fukwe za maziwa makubwa ikiwemo ziwa Victoria aidha mmomonyoko wa undogo kando ya fukwe ulimeripotiwa kuongezeka siku hadi siku katika mikoa ya Dar- es-salaam,Mtwara ,Tanga ,Lindi , Mwanza,Pwani na Visiwa vya Zanzibar Hivyo amesisitiza kuwa tabia hizo zikiendelea na wasipokuwa na mipango ya kuhakikisha usimamizi mzuri na uelekezaji sahihi fukwe hizo zitatokomea na pengine ata kumezwa na maji .
“Ninawasihi sana viongozi , wataalamu,wadau mbalimbali na watanzania wote kila mmoja kwa nafasi yake tufanye kila linalowezekana kuzinusuru fukwe zetu,ni vizuri tuwe na mijadala mipana mbayo itachangia kuleta mabadiliko chanya na kuisaidia serikali kuimarisha mifumo yake ya kisera,kisheria na kitaasisi ili kuweza kuboresha misingi ya usimamizi utuzanji na uwekezaji bora wa fukwe,”ameeleza Dkt Mpango.
Aidha ameeleza kuwa washiriki wa jukwaa hili watumie fursa hiyo kwa ajili ya kubadilisha maarifa na ujuzi kuhusu matumizi ya rasilimali na kubadili mitazamo juu ya namna bora ya kuwekeza katika fukwe za bahari,ziwa na mito ili kuleta faida za kiuchumi na kukuza mchango wake katika pato la taifa na maendeleo ya nchi.
“Mada hii imekuja wakati muafaka,kutokana na hivi sasa kama taifa tunaweka mkazo mkubwa katika kuendeleza uchumi wa bluu,hatuna budi kuchangamka na kuwa wabunifu kwenye suala hili,sisi viongozi, wataalam na wawekezaji tujadili kwa pamoja mambo ya kutunza, kusimamia na kuwekeza katika sekta hii adhimu ya fukwe ili iweze kuongeza mchango wake kwenye maendeleo ya nchi,”ameeleza Dkt.Mpango.
Sanjari na hayo Makamu huyo wa Rais,ameeleza kuwa suala la uhifadhi na usimamizi wa mazingira nchini ni moja ya vipaumbele muhimu vya serikali ambayo dhamira yake ni kuhakikisha maendeleo endelevu ya taifa kwa kuzingatia malengo ya dira ya maendeleo ya taifa 2025 inayolenga kufikia uchumi wa taifa tukiwa na kipato cha kati na maisha bora kwa kila mwananchi.
“Lazima tuzingatie matumizi bora ya ardhi na utunzaji wa mazingira kwa faida yetu na vizazi vyetu,mpango wa tatu wa maendeleo ya taifa ya miaka mitano pamoja na mikakati ya kisekta na ilani ya CCM vyote vimelenga kuchochea sekta binafi kuwa wakuza uchumi wa taifa na kuleta maendeleo kwa watanzania,”
Ofisa Mtendaji Mkuu kutoka Taasisi ya UONGOZI Kadari Singo,ameeleza kuwa jukwaa hilo ni la nane kufanyika tangu lilipo zinduliwa na ni moja ya programu kuu za Taasisi ya UONGOZI katika masuala ya maendeleo endelevu.
Lengo lake ni kukuza uelewa wa masuala ya uchumi wa kijani na mchango wake katika maendeleo nchini na linawakilisha zana ya kimaendeleo ya kujenga miunganisho ya kisekta, kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na kutunza mifumo ya ikolojia na mazingira.
Pamoja na kuelimishana na kukumbushana namna ya kutunza mazingira na kufanya uwekezaji wenye tija ili kutoa fursa za vizazi vijavyo kunufaika na uwepo wa fukwe.
Akizungumza katika kongamano hilo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja ameeleza kuwa serikali itaendelea kutunza fukwe ili zitumike kama sehemu ya utalii.
Ameeleza kuwa watu wengi wanafanya utalii za fukwe katika maeneo mbalimbali na kwamba lazima suala la usafi lizingatiwe kwa ajili ya kuzisafisha.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratias Ndejembi, ameeleza kuwa Taasisi ya Uongozi itaendelea kutoa mafunzo na elimu mbalimbali kwa wananchi na viongozi ili kuhakikisha fukwe na mazingira yanatunzwa.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza Reuben Sixbert,ameeleza kuwa fukwe nchini zina matatizo mengi ikiwemo uchafu,hivyo wanahusika wataona namna gani ya kuondokana na changamoto hiyo kwani lengo ni kutunza mazingira kwa ajili ya vizazi vijavyo.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa