Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Zanzibar
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa ushindi wa kishindo aliyoupata katika Uchaguzi Mkuu, Oktoba 2025.
Makamu wa Rais ametoa pongezi hizo wakati akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Zanzibar, amesema, ushindi huo ni matokeo ya kazi kubwa aliyofanya Dkt. Mwinyi pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Aidha kwa upande wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amempongeza Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi, kwa kushika wadhifa huo, na kumuhakikishia kuendelea kufanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Makamu wa Rais katika kutafuta ufumbuzi wa masuala mbalimbali ya kimuungano.

Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi, amefanya mazungumzo na Rais huyo wa Zanzibar lengo likiwa ni kujitambulisha.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi