December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makamu wa Rais ataka miradi ya maji kukamilishwa Mkoani Kilimanjaro

Na Mwandishi wetu,Timesmajira Online, Kilimanjaro

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameitaka Wizara ya Maji kuhakikisha mradi wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe pamoja na miradi ya maji inayotekelezwa wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro inakamilishwa .

Mhe. Mpango ametoa maelekezo hayo wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro.

Awali akitoa salam za Wizara ya Maji, Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amesema serikari inaendelea na utekelezaji wa miradi mitatu wilayani Rombo ambapo shilingi Bilioni 10 zimepangwa kutekeleza miradi hiyo.

Hata hivyo Mhandisi Mahundi ameitaja miradi hiyo kuwa ni mradi wa maji wa Njoro, Mradi wa maji wa Woma-Marangu pamoja na mradi wa maji wa Manda.

Aidha amewapongeza wananchi wa Kilimanjaro kwa kutunza vyanzo vya maji.