January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar,viongozi mbalimbali wapokea mwili wa Hayati Mwinyi

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online Zanzibar

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman,jioni ya leo Machi 01, 2024, amejumuika pamoja na viongozi mbalimbali katika hafla ya kuupokea Mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Hayati Ali Hassan Mwinyi.

Viongozi hao ni pamoja na wa Kitaifa wa Serikali, dini na Wanasiasa Mashuhuri, Viongozi Wastaafu, Mabalozi, Wanadiplomasia, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, familia na wananchi,

Hafla hiyo ambayo imefanyika katika uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume Zanzibar, imeongozwa na Mgeni Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na kuhudhuriwa pia na Rais wa Zanzibar Dokta Hussein Ali Hassan Mwinyi.

Katika hafla hiyo, Mheshimiwa Othman ameambatana na Mke wake, Mama Zainab Kombo Shaib.