December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar,aendelea kuwajulia hali wananchi

Na Mwandishi wetu timesmajira

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo Othman Masoud Othman, leo Jumatatu Machi 25, 2024, ameendelea na ziara Maalum ya kuwatembelea na kuwajulia-hali, Wagonjwa na Wazee mbali mbali wasiojiweza.

Katika ziara hiyo pia ametoa mkono wa pole kwa Wafiwa wa maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Mjini Unguja Kichama.