
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, Leo Februari 21, 2024 amefika na kutoa Mkono wa Pole kwa Familia ya Marehemu Mzee Kombo Ame, huko Garagara kwa Mbumbwini, Wilaya ya Magharib ‘A’ Unguja.
Marehemu Mzee Kombo ambaye ni Baba Mzazi wa Mmoja wa Wasaidizi wa Makamu, alifariki Dunia mapema usiku wa kuamkia juzi Februari 19, 2024 katika Hospitali ya Global, Mjini hapa.
Othman ambaye katika Ziara hiyo ameambatana na Mke wake, Mama Zainab Kombo Shaib, amewataka Wanafamilia kuwa na moyo wa subra katika kipindi hiki kigumu, sambamba na kuwataka kuzidisha Dua za Kumuombea Marehemu.
Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi, Amiin!


More Stories
Simbachawene:Mfumo wa Tathmini ya Mahitaji Rasilimaliwatu umebaini upungufu wa watumishi 441,366
Wakazi Arusha watakiwa kuchangamkia fursa huduma jumuishi za kifedha
Wahitimu wa Mafunzo ya Scout Nkasi watakiwa kuwa mwangaza kwa vijana