January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar ashiriki mkutano mkuu wa chama chake

Na Mwandishi Wetu,TimesmajiraOnline,

MAKAMAU Mwenyekiti wa ACT – Wazalendo Zanzibar ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Othman Masoud Othman, leo Jumanne Machi 05, 2024 amejumuika pamoja na Viongozi wengine, na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho, kwenye Mkutano Mkuu wa Taifa huko katika Ukumbi wa Mlimani City, Jijini, Dar es Salaam.

Mkutano huo wa Kikatiba, unatarajia pia Kuwachagua Viongozi wa Ngazi mbali mbali za Kitaifa watakaohudumu kwa Kipindi cha Miaka Mitano.

Viongozi mbali mbali wa  Siasa, Dini, Jamii, Mabalozi, Wanadiplomasia, na Watu Mashuhuri kutoka ndani na Nje ya Nchi, wamehudhuria katika Ufunguzi wa Mkutano huo wa Siku Mbili, sambamba na Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mama Zainab Kombo Shaib,wakiongozwa na Kiongozi Mkuu wa Chama hicho anayemaliza Muda wake swa Uongozi, Ndugu Zitto Zuberi Kabwe.