April 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar ahitimisha ziara yake

Na Mwandishi wetu, timesmajira

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, amekamilisha ziara Maalum ya kuwatembelea na kuwajulia-hali, Wagonjwa na Wazee mbali mbali wasiojiweza na pia kuwapa mkono wa pole wafiwa wa maeneo mbali mbali ndani ya Mikoa 11 ya kichama katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Othman ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo, alianza ziara hio Machi 19, mwaka huu katika Mkoa wa kusini Unguja na kumaliza leo katika Mkoa wa kichama wa Magharib B.

Ziara hiyo iliyoasisiwa na mtangulizi wake Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad, imewajumuisha pia Viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali, waliombatana na Othman, wakiongozwa na Katibu wa Idara ya Habari na Uenzezi wa ACT Wazalendo, Salim Biman.