Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman,jioni ya Septemba 1, 2024 ameitembelea na kutoa mkono wa pole kwa familia ya Almarhum Hawa Mairo,ambaye ni mama wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Batilda-Salha Buriani, alifariki dunia,mapema Agosti mwaka huu.
Ambapo Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,ametoa mkono wa pole kwa familia hiyo,nyumbani kwao marehamu huyo,Momela-Tanzanite, Wilaya ya Arumeru, Mkoa wa Arusha.
Othman yupo Jijini Arusha, kwa ajili ya ziara ya siku mbili,inayohusisha shughuli mbalimbali za jamii na serikali.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme
Mama Zainab:Watoto yatima ni jukumu la jamii yote