Na Mwandishi wetu, timesmajira
Makamu Mwenyekiti wa ACT – Wazalendo Zanzibar ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, leo Jumatatu Machi 04, 2024 amejumuika pamoja na Viongozi wengine Wakuu wa Chama hicho, katika Kikao cha Halmashauri Kuu, huko katika Ukumbi wa Hakainde Hichelema, Makao Makuu ya ACT- Wazalendo Magomeni Mikumi, Jijini, Dar es Salaam.

Kikao hicho cha Halmashauri Kuu, ambacho kimeongozwa na Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo Taifa, Ndugu Juma Duni Haji, ni katika muendelezo wa vikao kuelekea Mkutano Mkuu wa Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 5 na 6 mwezi Machi.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Kiongozi wa Chama, Makamu Mwenyekiti ACT Wazalendo Bara na Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ndugu Zitto Zuberi Kabwe, Doroth Semu na Ado Shaibu Ado.
More Stories
Ussi awataka wananchi Handeni kulinda miundombinu ya maji
Wapambe waanza rafu za uchaguzi Morogoro Mjini
Daraja la J.P.Magufuli kuzinduliwa Juni 19,2025