Na Penina Malundo, timesmajira
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Januari Makamba amesema serikali inatambua umuhimu wa wananchi kushiriki katika maamuzi yanayohusu masuala ya kitaifa na kimataifa ikiwemo utoaji wa maoni kuhusu marekebisho ya sera mpya ya mambo ya nje ya mwaka 2001.
Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam,wakati akifungua kongamano la kukusanya maoni ya wadau mahsusi kuhusu mapendekezo na marekebisho ya sera mpya ya mambo ya nje ya mwaka 2001.
Amesema kuna umuhimu wa wadau mbalimbali kushirikishwa kutoa maoni yao mahsusi katika mchakato wa marekebisho ya sera mpya ya mambo ya nje ya mwaka 2001.
Amesema Tanzania kama yalivyomataifa mengine,ambayo nchi zao zinavyokabiliwa na fursa na changamoto katika ushiriki wake kwenye jukwaa ya kimataifa.”Ni vema kuwa na sera madhubuti ambayo ni muhimu katika kutumia ipasavyo fursa hizo na kukabiliana na changamoto ambazo zitajitokeza,”amesema na kuongeza
”Kuna umuhimu wa maoni mbalimbali yanayotolewa na wadau katika kuwezesha uwepo wa sera yenye tija ,itakayokidhi matarajio ya wananchi,”amesema.
Makamba amesema kuna umuhimu wa kupata maoni ya sera hiyo ili kuwezesha taifa kunufaika ipasavyo na fursa zitokanazo na ushirikiano wa kikanda na kimataifa hasa utekelezaji wa dhana ya diplomasia ya uchumi.
Aidha amesema ndani ya kongamano hilo wadau hao watapata fursa adhim ya kuelewa kwa kina masuala muhimu yaliyomo katika sera ya mambo ya nje ikiwemo misingi ya sera zao na malengo yake.
”Pia wataweza kupata uelewa wa historia ya sera ya mambo ya nje tangu uhuru hadi 2001 ambapo utekelezaji wa sera kuanzia mwaka 2001 hadi sasa mapitio ya sera hiyo,”amesema.
Makamba amesema katika kongamano hilo,wizara yake inapenda kusikia kutoka kwa wadau jinsi wanavyoona marekebisho yaliyofanyika katika sera na ni maoni gani waliokuwa nayo kuhusu njia zitakazochukuliwa kufikia malengo wanayotamani kufikia.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â