Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline, Rukwa
KATIBU wa Halmshauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadiz Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, amesema Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendeleza miradi yote iliyoachwa na Hayati Rais Magufuli.
Makalla amesema hayo katika mkutano wa ndani wa viongozi na wanachama wa CCM mkoani Rukwa, kwenye ukumbi wa Nazareti mjini Sumbawanga.
Makalla ameongeza kwamba hakuna hata mradi uliosimama na pia Rais Samia ameanzisha miradi mipya mingi ya kimaendeleo ambayo yote utekelezaji wake umeendelea ipo ambayo imeshakamilika kwa asilimia 100.
“Katika hotuba ya kwanza ya Rais Dkt. Samia aliwahi kusema ‘kwakuwa alikuwa Makamu wa Rais wa aliyemtangulia Hayati Magufuli, anaelewa miradi yote kwakuwa walipanga pamoja’ na Rais Samia akawaahidi Watanzania atakamilisha miradi yote na hakuna hata mmoja utakaoachwa,” Alisema Mwenezi Makalla.
Makalla ameendelea kusema kuwa Rais Samia ametekeleza hilo kwa asilimia 100 na ameanzisha miradi mipya mingi yenye kunfaisha katika sekta za Elimu, Afya, Maji na Miundombinu.
“Hapa Rukwa mmependelewa sana kwakuwa maendeleo yanakwenda kwa kasi…awamu nyingi zimepita lakini hapakuwa na ujenzi wa uwanja wa ndege ila awamu ya sita chini ya Rais Samia amekata mzizi wa fitina na kuanza ujenzi wa uwanja wa ndege wa Sumbawanga na kwa maelekezo ya Katibu Mkuu wetu Dkt. Nchimbi kwa wakandarasi amewambia hatutaki utani na uwanja ukamilike kwa haraka…mwakani CCM tuna jambo letu na kukamilika kwa uwanja huu wananchi wa Rukwa watanufaika kwa kupata wateja wa kimataifa,” amesisitiza.
More Stories
Balozi Nchimbi kuongoza waombolezaji mazishi ya Kibiti leo
Dkt.Tulia,apewa tano kuwezesha wananchi
Nkasi yajipanga kukusanya mapato