Na Agnes Arcado, TimesMajira Online, Dar es Salaam
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA. Amos Makalla, amesema ameridhishwa na utulivu na amani iliyopo katika vituo vya kupigia kura na kuendelea kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi leo kwenda kupiga kura katika vituo vyao
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika kituo cha kupigia kura kilichopo Mtaa wa TPDC, Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, baada ya kupiga kura ya kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa ikiwemo Mwenyekiti na Wajumbe wa Serikali za Mitaa, Makalla ameonesha kuridhishwa na hali ya utulivu inayoendelea katika vituo vya kupigia kura vilivyopo maeneo mbalimbali.
“Mimi tayari nimeshatimiza haki yangu ya msingi ya kuwapigia kura viongozi wangu wa mtaa na hali niliyokutana nayo hapa na maeneo mengine inaridhisha ni hali ya utulivu na amani, hivyo nitoe rai kwa wananchi wote kujitokeza kwa wingi katika vituo vyao ili watimize haki yao ya msingi kwa kuwachagua viongozi wao wa Mitaa”, amesema CPA. Makalla.
Aidha, CPA. Makalla ameeleza kusikitishwa na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni Dkt. Faustine Ndugulile, aliyefariki usiku wa kuamkia leo Novemba 27, 2024 akiwa nchini India kwa matibabu.
More Stories
Nani kuwa mrithi wa Kinana CCM?
Watendaji Songwe wapatiwa mafunzo uboreshaji daftari la mpiga kura
Samia: Mwaka 2024 ulikuwa wa mafanikio