Judith Ferdinand, Timesmajira Online,Mwanza
Makada wanne wa Chama cha Demkokrasia na Maendeleo(CHADEMA), wakiwemo mawakala wawili wamekatwa na Jeshi la olisi mkoani Mwanza kwa tuhuma za kukimbia na karatasi za kupigia kura pamoja na kufanya fujo kwenye kituo cha kupigia kura.
Akizungumza na waandishi wa habari Novemba 27,2024,mkoani hapa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa,amesema,matukio machache ambayo yamejitokeza na jeshi hilo likachukua hatua katika zoezi la upigaji kura ni pamoja na Novemba 27,2024 majira ya saa moja na nusu asubuhi,Wilaya ya Nyamagana katika kituo cha kupigia kura cha Lwan’hima mtaa wa Maliza,kituo hicho ambacho kipo shule ya sekondari Lwan’hima pamoja na kituo hicho pia kulikuwa na vituo vingine vya kupigia kura.Ambapo muda huo kulikuwa na mawakala wa CHADEMA na Chama Cha Mapinduzi(CCM),vyama hivyo vilikuwa na wagombea.
“Muda huo nilioutaja wakala wa CHADEMA aliyejulikana kwa jina la Edward Odingi,aliyekuwa kweye kituo hicho wakati huo,alianza kuwasiliana na mgombea wa Uenyekiti kupitia CHADEMA alijulikana kwa jina la Athanas Ndaki.Mgombea huyo alipofika kwenye kituo katika hali ya kushangaza wakala huyo wa CHADEAMA,alichukua boksi ambalo lilikuwa na karatasi za kupigia kura,na kuondoka nazo akiwa ameungana na Ndaki(mgombea),”amwsema Mutafungwa na kuongeza:
“Askari wa Jeshi la Akiba aliyekuwa katika kituo hicho, alishangaa kuona wakala anafanya kitendo hicho na kuanza kumfukuza kisha kutoa taarifa kwa asakari wetu waliokuwa doria jirani na kituo hicho,walifanikiwa kumkata wakala huyo na mgombea huyo wakiwa na karatasi za kupigia kura 181, ambazo zilikuwa hazijapigwa muhuri kwa sababu muda huo zoezi la kupiga kura lilikuwa halijaanza.Kwani zoezi la kupiga kura lilianza saa 2 kamili asubuhi wakati tukio hilo likitokea saa moja na nusu asubuhi,”.
Sanjari na hayo katika tukio hilo pia walimkata Ally Hussein ambaye ni wakala wa CHADEMA kituo cha Lwanhima”A”,ambacho ni jirani na kile tukio lilipotendeka tukio hilo,huku wakiendelea na mahojiano na watuhumiwa hao na kuzifanyia uchunguzi karatasi hizo.Ambalo baada ya tukio hilo hali ya usalama iliendelea kuimarishwa na zoezi la kupiga kura liliendelea vizuri.
Mutafungwa amesema pia majira ya saa 2:45,asubuhi jeshi hilo lilimkamata Amos Ntobi(34) Katibu wa CHADEMA ngazi ya Wilaya mkazi wa Mabatini wilayani Nyamagana, kwa tuhuma za kufanya fujo katika kituo cha kupigia kura cha Kabengwe kilichopo mtaa wa Mabatini.
“Alikuwa hakifanya fujo akidai kuwa kituo hicho akipo kwenye orodha ya vituo vya kupigia kura katika mtaa huo,hivyo alikuwa akiwazuia watu wasiende kwenye kituo hicho.Tumeona kitendo hicho ni kati ya vitendo vinavyokatazwa kwa mujibu wa sheria,na anaendelea kuhojiwa na ulinzi uliimarishwa na kuwapa nafasi watu walikuwa wanataka kupiga kura,”.
Awali Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Jiji la Mwanza Wakili Kiomoni Kibamba,amesema,kuhusu malalamiko ya vituo zaidi vya kupigia kura ni upotoshaji,ambapo amefafanua kuwa CCM ilileta idadi ya mawakala 1011, CHADEMA 1025, kulingana na dadi ya vituo na vyama vilivyobaki pia vilileta mawakala wao,huku akidai kuwa CHADEMA ilipeleka zaidi.
Amesema, katika hali ya kushangaza CHADEMA, walilazimisha wagombea wao kuwa mawakala kinyume na matakwa ya kanuni ndogo ya 6 ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
Kwa upande wake Msimamizi wa Uchaguzi wa Ilemela,Ummy Wayayu,amesema katika jimbo hilo hali ni shwari, hakuna changamoto kuhusiana na uchaguzi kwani licha ya mvua kunyesha maeneo mbalimbali bado wananchi wameitikia na kujitokeza kupiga kura kwa amani, haki na uhuru.
More Stories
Wanaoficha watoto wenye ulemavu kusakwa
Mawakili Tabora walaani kuziwa kutekeleza majukumu
RC Mrindoko:Ufyekaji wa mahindi Tanganyika si maelekezo ya serikali