December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Majizzo afunguka kuhusu ndoa yake na Lulu

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MKURUGENZI wa E-FM na TV-E Majizzo, kwa mara ya kwanza amefunguka juu ya ndoa yake na Muigizaji wa Filamu hapa nchini Elizabeth Michael maarufu kama ‘Lulu’, kwanini ndoa yake ilikuwa kwa mshangao ‘surprise’ na kwanini ilikuwa ya watu wachache.

Akiweka wazi hilo leo, kupitia kipindi kipya cha Joto Kali la Asubuhi kinachoendeshwa na Mtangazaji Gerald Hando, Majizzo amesema, alitaka kuwaonesha vijana kwamba unaweza kufunga ndoa hata kama una kitu kidogo.

“Mimi ningeweza kuwa na watu zaidi ya elfu 3 lakini nilitaka nisiwatishe, harusi haikuwa ya gharama (ukiachilia mavazi). Lakini pia nilitaka kufanya jambo la kiroho tu. Wazazi walitupa ‘support’ kubwa. Mimi nina marafiki wengi ningetaka kuchangisha wangejaa, Elizabeth Michael naye ana marafiki wengi BongoMovie yote wangejaa,” amesema Majizzo.

Itakumbukwe, Februari 16, mwaka huu, Muigizaji Lulu alifunga ndoa na mchumba wake ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji (CEO), wa EFM na TVE, Francis Antony Ciza maarufu ‘Majizzo’ katika Kanisa Katoliki la Mt. Gasper, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

%%%%%%%%%%%%%%