Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online
MUANDAJI wa Tamasha la Shukrani kwa Mungu Alex Msama leo ametagaza majina ya waimbaji ambao watashiriki katika tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Octoba 31 mwaka huu, katika Viwanja vya Uhuru Jijini Dar es salaam.
Waimbaji hao ni pamoja na Boniface Mwaitege, Upendo Nkone, Christopher Mwagila, ambapo tayari wameishaingia kambini kwa maandalizi ya tamasha hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam mapema leo, Msama ambaye pia ni Mkurungezi wa Kampuni ya Msama Promotion ambao ndio waandaji wa tamasha hilo amesema kwa sasa maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri.
Amesema, hadi sasa waimbaji mbalimbali wamezidi kujitokeza kwa ajili ya kushiriki katika tamasha hilo ambalo litakuwa ni la kiistoria.
“Waimbaji ni wengi na wameendelea kujitokeza kutoka ndani ya na nje ya nchi, tamasha hili litakuwa la kiistoria na tumejipanga vizuri kuhakikisha wananchi hawatojutia kufika uwanjani kwa burudani watakayoipata,” amesema Msama.
Aidha amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo la kihistoria ambalo limebeba ujumbe wa kumshukuru Mungu na kuliombea Taifa kwa ujumla.
Naye mratibu wa Tamasha hilo, Emmanuel Kabisa amesema tamasha litakuwa la tofauti na miaka mingine ambapo Kampuni ya Msama Promotion imetoa fursa kwa wananchi kupiga kura kwa ajili ya kuwachangua waimbaji wa kizazi kipya wanaoweza kuimba Nyimbo za Injili .
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio