Na.Mwandishi Wetu, Timesmajira Online, Mtwara
Serikali imesema kuwa kwa mwaka 2023 imeendelea kuboresha huduma za afya kwa kujenga jumla ya majengo 128 ya huduma za dharura pamoja na majengo 78 ya huduma za wagonjwa mahututi nchi mzima.
Hayo yameelezwa leo na Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel,Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara katika ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan wakati akisalimia wananchi wa wilaya hiyo.
“Kwa mwaka huu serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imejenga majengo ya huduma za dharura 128 nchi nzima na majengo ya huduma za wagonjwa maututi 78 ili kusaidia wananchi kupata huduma hizo kwa urahisi,”amesema Dkt. Mollel
Dkt. Mollel amesema sekta ya afya yote kwa mwaka huu imepewa trilioni 6.7 huku mashine za X-RAY za kisasa 199 zimenunuliwa na kusambazwa katika hospitali kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi ambapo X-Ray moja ya kisasa inagharimu kiasi milioni 500.
Pia amesema kuwa serikali imemsaidia kupunguza rufaa za kwenda nje ya nchi kwa kuwezesha sekta ya afya kutoa huduma za sikoseli katika hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma na hospitali ya Mifupa (MOI) iliyopo jijini Dar es Salaam kwa kuwa na mashine yenye uwezo wa kufanya upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye sakafu ya ubongo kupitia puani.
“Mashine hiyo ya kufanyia upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye sakafu ya ubongo kupitia puani imegharimu kiasi cha bilioni 21 hiyo ni ishara ya upendo wa Rais Dkt. Samia kwa watanzania katika kulinda afya za Watanzania wasipate adha ya huduma za matibabu,”amesema Dkt.Mollel
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â