February 3, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Majaliwa:Serikali imejipanga kukamilisha maandalizi michuano CHAN,AFCON

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online, Dodoma

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imejipanga vyema kukamilisha maandalizi yote muhimu ikiwemo miundombinu kwa ajili ya Michuano ya Mpira wa Miguu kwa Nchi za Africa (CHAN) na AFCON.

Akifungua tamasha la Michezo la Bunge Bonanza February Mosi mwaka huu katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya John Merlin jijini Dodoma ambalo liameandaliwa na benki ya Azania Waziri Mkuu Majaliwa amesema ,Tanzania imejipanga vizuri, kuhakikisha kuwa michuano hii inafanyika hapa Nchini, kwa kuandaa miundomvinu yote muhimu .

“Tayari ukaguzi wa baadhi ya viwanja umefanyika na vimeonekana kukidhi vigezo “Viwanja vilivyokaguliwa vipo Tanzania bara na Visiwani, na kazi bado inaendelea, lengo ni kuhakikisha michuano hii inafanyika kwa ufanisi” amesema Waziri Mkuu na kuongeza kuwa

“Ni vyema sasa Watanzania wakajipanga kutumia fursa zitakazo jitokeza kutokana na kuwepo kwa michuano hiyo hapa Nchini na kuongeza fursa za kiuchumi

Amesema ni fursa kwetu Watanzania, lazima tujipange kutumia fursa za kiuchumi zitakazojitokeza, ili tuweze kunufaika”.

Aidha,Waziri Mkuu Majaliwa ametumia nafasi hiyo kumpongeza Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson kwa kuandaa Tamasha la Michezo la Bunge Bonanza ambalo limewakutanisha wabunge na wanamichezo mbalimbali wa Mkoani Dodoma.

Akifunga bonanza hilo,Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Walles Karia amepongeza
jitihada za Bunge kwa kusapoti jitihada za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan za kupunguza magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

“Na sisi kama Shirikisho tumekuja kwani tumejua hili ni jambo muhimu la kuunga mkono michezo ikiwemo inayopendwa Dunia nzima lakini pia kushirikisha viongozi na mashabiki wa timu kongwe za Simba na Yanga

Naye Mwenyekiti wa Klabu ya michezo ya Bunge Festo Sanga bonanza hilo limeshitikisha Wadau mbalimbali ambao ni mashabiki wa Yanga wakiwemo viongozi wa timu hizo Kongwe,jogging na Wabunge.

Wadau wengine walioalikwa katika bonanza hilo ni Hospitali ya Benjamin Mkapa,Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DUWASA),Wizara ya Maji, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF ),Chuo Cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) ,Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ,Shule ya sekondari ya John Merlin na wanafunzi wake ambalo bonanza hilo linmefanyika

Aidha amesema dhima na maono ya spika kuanzisha bonanza ni pamoja na kufanya mazoezi kupambana na mgonjwa yasiyo ya kuambukiza.