December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Majaliwa:Nimefurahi kuona Jeshi la uhamiaji wanashiriki gwaride kwa mara ya kwanza

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amefurahishwa na kitendo cha Jeshi la uhamiaji kushiriki kwa mara ya kwanza gwaride kwajili ya  siku ya kumbukumbu ya Mashujaa yanaoyoadhimishwa kila ifikapo Julai 25 kila mwaka.

“Nimefurahishwa kuona gwaride la jeshi la uhamiaji kwa mara ya kwanza linashiriki ninaimani kuwa Jeshi hili litaendelea kuonekana kwenye magwaride kwenye shughuli zetu za kitaifa,”amesema Waziri Mkuu.

Majaliwa amesema hayo jijini hapa leo alipotembelea eneo litakazofanyika sherehe za kumbukumbu kwajili ya kukagua maandalizi ya sherehe hizo ambazo zitafanyika kitaifa Mkoani hapa.

“Nimeridhishwa na maandalizi haya kwani ni kweli wazi maandalizi yapo vizuri  kamati tendaji kupitia kurugenzi ya maandalizi imefanya kazi kubwa na ya kukubalika kwani tumeshuhudia vikundi vya majeshi vikiongozwa na gwaride vikiwa vipo katika ukakamavu wa hali ya juu,”amesema Nakuongeza,

“Tumeona Matukio yameenda Kama ratiba ilivyopangwa na kesho kamati itaendelea kuthibitisha washiriki watakaokuja katika sherehe hizi za Mashujaa na tunaimani hadi kufikia tarehe 25 tutakuwa tumeshapata idadi ya washiriki wote,”amesema Majaliwa.

Pamoja na hayo amisisitiza ofisi ya Mkuu wa Wilaya kuendelea kuhamasisha wananchi kujitokeza katika maadhimisho ya Sherehe hizo huku akiitaka Ofisi ya maadhimisho iliopo katika Ofisi yake kuendelea na maboresho zaidi na madogo madogo  katika viwanja hivyo.